Advertisements

Tuesday, August 23, 2016

TAARIFA KUTOKA UBALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA KUHUSU OPERESHENI UKUTA

Ubalozi wa Marekani kwa Tanzania umewatahadharisha raia wa Marekani waishio nchini kuhusiana na Operesheni UKUTA iliyopangwa kufanyika septemba.

Taarifa kutoka ofisi za ubalozi huo zinaeleza kuwa kuna hofu ya maandamano hayo kudumu hata baada ya september mosi hivyo kuwataka raia wake kuwa makini na usalama wao.

Ubalozi umeeleza kuwa raia wa Marekani hawajawai kuwa wahanga wa maandamano yaliyopita ila umewataka raia wake kuwa makini juu ya usalama pamoja na kufuatilia vyombo vya habari vya ndani ili kujua kinachoendelea.

Ubalozi huo umesema ingawa maandamano yamedhamiriwa kuwa ya amani, kuna uwezekano wa kutotokea makabiliano yatakayoweza kusababisha machafuko hivyo kuwataka raia wake kuepuka maeneo yatakayokuwa na maandamano. 
**************
Security Message: Nationwide Protests Scheduled for September 1, 2016

The U.S. Embassy in Dar es Salaam alerts U.S. citizens that opposition political leaders have called for a nationwide day of protest currently scheduled for September 1, 2016, but may continue for more than one day.

While U.S. citizens have not been specifically targeted in past demonstrations, we urge you to exercise caution and stay current with media coverage of local events.

Even demonstrations intended to be peaceful can turn confrontational and escalate into violence.  Avoid areas where demonstrations are taking place and exercise caution when in the vicinity of any large gatherings, protests, or demonstrations.

For further information:
  • Contact the U.S. Embassy in Tanzania, located at 646 Old Bagamoyo Rd, Msasani, Dar es Salaam, at+255-22-229-4000 or e-mail at drsacs@state.gov, and is open Monday-Thursday, 7:30 a.m.-5:00 p.m and Friday 7:30 – 11:30 a.m. For after-hours emergencies, U.S. citizens should call +255-22-229-4000 and ask to speak with the duty officer.
  • Call 1-888-407-4747 toll-free in the United States and Canada or 1-202-501-4444 from other countries from 8:00 a.m. to 8:00 p.m. Eastern Standard Time, Monday through Friday (except U.S. federal holidays).

2 comments:

Anonymous said...

Hivi ndivyo mataifa fulani yanavyofurahia na kukimbilia kutangaza habari chafu za kiafrika. Tanazania kuna mengi mazuri na kuyafurahisha yametokea hapo hukuwahi kumsikia huyo balozi akiwatangazia watu wake na dunia leo kasikia harufu ya machafuko hata hayajatokea tayari anaitangazia dunia Tanzania kuna matatizo. Sina uhakika lakini sidhani kama kuna mmarekani amepoteza uhai wake kwa sababu za kiusalama nchini Tanzania katika miaka ya karibuni ukilinganisha na vifo kazaa vya watanzania waliopoteza maisha yao nchini marekani hivi karibuni kwa sababu za kiusalama na hatukuwahi kumsikia balozi wa tanzania akiwatahadharisha na kuitangazia dunia kutokana na hali mbaya ya usalama nchini marekani. Tanzania ni nchi yenye stable government na vyombo vya usalama vya uhakika nashindwa kuelewa huyo balozi ana lengo gani kwa nchi yetu. Maandamano na shughuli nyengine za kisiasa ni mambo ya ndani ya Tanzania yeye kama balozi serikali ya Tanzania lazima itamwakikishia usalama wa watu wake kwani Tanzania sio Burundi kitendo cha kutoa tahadhari kana kwamba hapo nyuma watu wake wameshahikuwa wahanga wa shughuli za kisiasa Tanzania ni cha kushangaza.

Anonymous said...

Acha kuwa mjinga wewe. Balozi wa Marekani anajali kuhusu raia wake na anapoona umuhimu wa kuwataadhalisha raia wake anafanya hivyo. Huyo balozi wenu wa Tanzania marekani hajakatazwa na mtu kuwataadhalisha wananchi wake. Tatizo lako wewe hapo juu unataka kufananisha kifo na usingizi. Marekani ni nchi kubwa maandamano yako kila siku hata huyo balozi hayajui, sasa hebu kaa kimya na usifananishe hayo maandamano ya tanzania na ya marekani. Na kwa taarifa yako Marekani inajali sana raia yake.