Advertisements

Sunday, September 25, 2016

MAONESHO YA UJASILIAMALI IRINGA YAFANA

Mkuu wa wialaya Mh Richard Kasesela akitoa hotuba wakati wa maonesho ya wajasiliamali aliyoyaandaa katika barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa.


Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza amefungua maonesho ya wajasiliamali yalioandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela katika barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa. 

Akifungu Maonyesho hayo, aliwaasa wana vikundi kuwa na umoja ili kufanikisha ndoto zao. Pia aliagiza benki ya Posta kuhakikisha wanawasaidia mikopo wajasiliamali hayo. 

Mapema akimkaribisha Mkuu wa mkoa , Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kumuomba maonesho hayo yawe yanafanyika mara kwa mara ili wajasiliamali wapate soko na kujikwamua kwa uchumi. 

Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Iringa Bwana Kayanda aliwambia wajasiliamali pesa ipo, ila wakopaji ndio hakuna hivyo anawakaribisha waje kukopa. 


Zaidi ya wajasiliamali 600 walipata mafunzo yaliyoandaliwa na Mh Kasesela hapo tarehe 18/8/16, na leo ilikuwa siku ya kuonyesha bidhaa hizo. 

Pia kilikuwepo kikundi ambacho kinatengeneza mipira ya kuchezea mpira wa miguu cha kata ya Ruaha.
Mkuu wa mkoa Bi Amina Msenza akipata maelezo kutoka kwa wajasiliamali baada ya ufunguzi wa amonyesho hayo.
Mkuu wa wilaya akicheza mpira uliotengenezwa na wajasiliamali wa Ruaha Iringa


No comments: