Advertisements

Tuesday, October 18, 2016

LEMA AZUA TAHARUKI UZINDUZI WA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHA LEO

Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru Broun
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.


VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).

Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .

3 comments:

Anonymous said...

Ushamba kitu kibaya sana. Mbunge na mkuu wa mkoa mnataka kupigania nini? Kama kuna tofauti ya sera mnazifanyia mdahalo siyo kupigana.

Anonymous said...

Africa haiwezi kuendelea kamwe kwa sababu ya viongozi kama huyu mkuu wa mkoa wa Arusha.Bara zima limejaa viongozi wa aina hii...Kwao siasa ndio Mungu wao...Uongo,Majungu, na unafiki ndio sera, Utaifa haupo...Kamwe huwa hawajui vyama vya siasa ni vya msimu tuu, ila Nchi ni ya kudumu....

Anonymous said...

Ni aibu kuwa na viongozi wasiozingatia leadership eethics hii si mara ya kwanza wananchi kushuhudia utovu wa nidhamu wa viongozi wetu.Juzi kati Msigwa alikaribia kukunja ngumu dhidi ya mkuu wa wilaya. Tanzania tunakwenda wapi?
Thanks mzee Mwinyi kwa kuliona hili na kusema nchi inakwenda"..