Advertisements

Sunday, October 2, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIOTUO CHA KUFUA UMEME MZAKWE MKOANI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (kushoto) kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme kwenye makao makuu ya nchi Dodoma wakati alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. Wengine Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Christina Mndeme.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanayakazi na viongozi wa kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha Dodoma wakti alipokitembelea mjini Dodoma Oktoba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uzalishaji katika kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha mjini Dodoma wakati alipokitembelea Oktoba 2, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa mkurugenzi wa kiwanda cha Magodoro Dodma, Haidary Gulamali, magodoro 200 yenye thamani ya shilingi milioni 10 ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Spring zinazotumika kutengeneza magoro wakati aliopotembelea kiwanda cha Magodoro Dodoma Oktoba 2, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha Magodoro Dodoma baada ya kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2, 2016. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali na kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na wapili kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama

No comments: