Advertisements

Sunday, November 13, 2016

DHAMANA YA LEMA KUJULIKANA KESHO

 Mbunge wa jimbo la Arusha, Godbless Lema(40) na Mkewe Neema Lema(33) wanatarajia tena kupanda kizimbani kesho kwa madai ya kesi ya uchochezi dhidi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Ijumaa wiki iliyopita Lema alipelekwa gereza la Kisongo Arusha, kutokana na kunyimwa dhamana, katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake.
Hata hivyo Chadema kinatarajia kuwasilisha maombi mahakama kuu, kuomba Lema apewe dhamana.
Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro, alisema jana kuwa hawakuridhishwa na pingamizi la dhamana lililowekwa na mawakili wa serikali wiki iliyopita kwani tayari Lema alikuwa amepewa dhamana na hakimu.
"Tayari tumefanya mazungumzo kuongeza nguvu za mawakili wa chama ambao wataungana na mawakili wa Arusha kudai dhamana leo"alisema.
Naye Wakili Shaki Mfinanga alisema kesho watawasilisha maombi ya dhamana ya Lema wakiwa na mawakili wa Chadema.
"Taratibu za kisheria zinaendelea tunatarajia jumatatu kuwasilisha pingamizi la Lema kunyimwa dhamana."alisemaNo comments: