ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 22, 2017

Mtu mmoja afariki katika shambulio kwenye Bunge Uingereza

Mshambuliaji akidhibitiwa
Mwanamke mmoja amethibitishwa kufariki katika eneo la Daraja la Westminster, katikati ya London katika kinachochukuliwa kuwa shambulio la kigaidi.

Afisa wa polisi alidungwa kisu katika majengo ya Bunge yaliyoko hapo karibu. Mshambuliaji huyo alipigwa risasi na polisi.

Mshambuliaji huyo alikuwa amevurumisha gari na kuwakanyaga watu katika daraja hilo kabla ya kuligongeza kwenye ua wa daraja hilo.

POlisi wamesema kuna "majeruhi kadha ... wakiwemo maafisa wa polisi" na kwamba "uchunguzi kamili wa kukabiliana na ugaidi" unaendelea.

Kiongozi wa bunge la Commons David Lidington aliwaambia wabunge awali kwamba "mtu aliyemshambulia polisi alipigwa risasi na polisi".

Wabunge wamesema kuwa walisikia milio mitatu ama minne ya risasi . Duru kutoka ofisi ya Waziri Mkuu ya Downing Streetzimesema kuwa Waziri Mkuu Theresa May yuko "Salama".

Waziri Mkuu Theresa May alionekana akisafirishwa kutoka ofisini kwake na gari la aina ya Jaguar wakati kile kilichosikika kama milio ya bunduki ilipokuwa ikiendelea kusikika kwenye bunge wakati wa tukio hilo.

Wahudumu ndani ya bunge waliambiwa wasalie ndani ya ofisi zao.

Tom Peck, mhariri wa masuala ya kisiasa wa gazeti the Independent, alituma ujumbe wa Twitter uliosema : "Kuna sauti kubwa . Kelele. mkanganyiko. Halafu sauti za risasi. Polisi waliojihami kila mahali."

Mhariri wa kisiasa wa shirika la habari la Press Association Andrew Woodcock alishuhudia tukio hilo lilivyokuwa likiendelea kupitia dirisha la ofisi yake lililo mkabala na New Palace Yard.

"Nilisikia kelele na vilio kutoka nje na nikaangalia , niliona kikundi cha watu labda kati ya 40 na 50 wakikimbia kutoka kwenye mtaa wa Bridge Street ndani ya medani ya Parliament.

"They appeared to be running away from something.

"Wakati kundi hilo lilipowasili katika lango la carriage, ambako polisi walikuwa wameshika doria , ghafla mwanamume mmoja alikimbia kutoka kwenye umati huo.

"Alionekana akiwa ameshikilia kisu cha jikoni mkononi.

"Nikasikia kile kilichosikika kama milio ya risasi - Nadhani wanaume watatu kati yao - na halafu kitu kingine nilichokifahamu ni kwamba kulikuwa na watu wawili waliokuwa wamelala chini na wengine wanaokimbia kuwasaidia.

"Polisi waliojihami walifika haraka kwenye eneo la tukio na nikasikia wakipaza sauti kuwaambia watu waondoke mbali na eneo la tukio''

Shahidi mmoja aliyeshuhudia tukio hilo , Radoslaw Sikorski, mhadhiri wa kituo cha Chuo Kikuu cha Havard kituo cha Mafunzo ya Ulaya , alituma video iliyoonyesha watu waliokuwa wamelala chini ardhini wakiwa wamejeruhiwa kwenye bara bara ya kuelekea Westminster Bridge.

Aliandika : "Bara bara katika Westminster Bridge imefungwa na watu watano."

Kituo cha polisi cha Scotland Yard kimesema kuwa kiliitwa kushughulikia tukio la ufyatuaji risasi katika eneo la Westminster Bridge na taarifa kwamba watu kadhaa wamejeruhiwa.

Huduma za usafiri mjini London zimetangaza kuwa safari za leri ya treni za treni za chini ya ardhi zimefungwa kufuatia ombi la polisi na mabasi yameagizwa kufuata njia nyingine.

Bwana Lidington amesema "Inaelekea afisa wa polisi amechomwa kisu, na mtu aliyemchoma kisu amepigwa risasi.

"Gari la ambilansi kwa sasa linawahudumia wagonjwa na kuwaondosha majeruhi eneo la tukio.

''Pia kuna taarifa zaidi za matukio ya ghasia katika kasri la Westminster lakini natumai wenzangu katika pande zote watataka nisizungumzie mengi zaidi hadi tutakapo pata taarifa kamili kutoka kwa polisi na kutoka maafisa wa usalama wa bunge juu ya kile kinachoendelea"

BBC

No comments: