ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 22, 2017

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA MASUALA YA UTAMADUNI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia) wakibadilishana mkataba wa makubaliano utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena ijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakiangalia zawadi. 
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakisaini mkataba huo.

Na Dotto Mwaibale


SERIKALI ya Tanzania na China zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020.

Nchi hizo zimetiliana saini za mkataba huo kupitia kwa Mawaziri wa wizara husika katika masuala ya utamaduni ambapo kwa China Naibu Waziri wa Utamaduni, Gong Wei alihusika katika tukio hilo.

Kwa Upande wa Tanzania Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alishiriki kutia saini.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, Gong Wei alisema kwa muda mrefu nchi ya China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika mambo mengi ikiwepo sanaa na utamaduni hivyo akaomba ushirikiano huo uendelee kudumu.

Alisema katika kudumisha ushirikiano huo Serikali ya China itatoa kiasi cha Yuan laki nne (400,000) kwa ajili ya kununua

samani kwa Wizara hiyo ambazo zitatumika katika maofisi ambapo alimuomba Waziri Nape kueleza ni samani gani zitakazo hitajika ili ziletwe.

Waziri Nape aliishukuru China kwa msaada huo na kusema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali.

Katika hafla hiyo mawaziri hao waliweza kupeana zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: