SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza
umeme cha Ilala jijini Dar es Salaam, kitakuwa kwenye maboresho makubwa Machi
26, 2017 na hivyo itapelekea eneo kubwa la jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Bi. Leila Muhaji
imesema umeme utakosekana kuanzia saa 3 asubuhi na kurejea saa 10 jioni ambapo
ametaja maeneo yatakayoathirika kufuatia kazi ya kuboresha kituo hicho ni
pamoja na eneo la katikati ya jiji, Upanga, Kariakoo, Buguruni, Ilala, Mbagala
na Chang’ombe.
Aliyataja
maeneo mengine kuwa ni pamoja na Kurasini, Kiwanda cha saruji Maweni, Wizara ya
Maliasili na Utalii, (Mpingo House),Tusiime Mission na Tanzania Oxygen. Mengine
yaliyotajwa ni pamoja na Ofisi ya Manispaa ya Temeke, Unilever, Mkuu wa Wilaya
ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jarmana Printers,
Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate, na maeneo jirani.
Bi.
Leila aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Goldstar, Quaim, Robbarac,
Simba Plastic, Veta, Duce, JKT Mgulani Barracks, Keko, Mkuranga,Chuo cha Diplomasia,
21st Century, Oilcom, Engen na eneo la Mtoni Mtongani.
21st Century, Oilcom, Engen na eneo la Mtoni Mtongani.
Aidha
kufuatia katizo hilo la umeme, TANESCO imetoa tahadhari kwa wananchikutoshika
nyaya za umeme zilizokatika na kwuataka watoe taarifa kwenye namba za dharura
za TANESCO.
Leila
alisema, uongozi wa TANESCO unaomba radhi kutokana na usumbufu utakaojitokeza
kutokana na kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment