Advertisements

Thursday, June 8, 2017

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AZINDUA ALBAMU YA KWAYA YA CECILIA MJINI MAFINGA

 Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akizindua albamu ya kwaya ya Cecilia katika kanisa la Katoliki la Mjini Mafinga akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve (kulia) wakati wanawasili katika kanisa la Katoliki la Mjini Mafinga.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve akiwa anawasalimia waumini wa  Kanisa Katoliki la Mjini Mafinga akiwa amembatana na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakati wa uzinduzi wa Albamu ya kwaya ya Cecilia iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba.
 Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve wakiwa wanatoa sadaka  katika  Kanisa Katoliki la Mjini Mafingawakati wa uzinduzi wa Albamu ya kwaya ya Cecilia iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve (kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakifuatilia misa katika  Kanisa Katoliki la Mjini Mafinga wakati wa uzinduzi wa Albamu ya kwaya ya Cecilia iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja  Mchungaji wa Kanisa Katoliki la Mjini Iringa Leornad Muli na viongozi mbalimbali wa jimbo la Iringa Mjini akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi (wa nne kulia), Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve

Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba amezindua albamu ya kwaya ya Cecilia uliofanyika katika Kanisa la Katoliki Mjini Mafinga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoani humo.

Katika uzinduzi wa albamu hiyo, Mwigulu aliweza kuchangisha harambee ya uzinduzi na kufanikiwa kupata milioni 25 na kuzidi kufanikisha mafanikio ya kwaya hiyo.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve amesema kuwa anamshukuru sana Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba kwa kuweza kuwatembelea na kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kufanikisha zoezi zima la uzinduzi wa kwaya ya Cecilia.

"Namshukuru sana Waziri  Mwigulu kwa kuweza kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kwaya ya Cecilia na kufanikisha zoezi zima ikiwemo kupatikana kwa milioni 25 ikiwa ni harambee ya uzinduzi,"amesema Rose.

Katika uzinduzi wa albamu hiyo baadhi ya viongozi mbalimbali waliweza kuwepo ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi na Mkuu wa Wilaya Mafinga Jamhuri William.

No comments: