Advertisements

Tuesday, July 4, 2017

DC Kinondoni aagiza Halima Mdee akamatwe, awekwe ndani kwa saa 48

Mkuu wa Wilaya (DC) Kinondoni, Ally Hapi amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda kumkamata mbunge wa Kawe, (Chadema) Halima Mdee na kumweka mahabusu kwa saa 48 kutokana na kutoa maneno ya uchuchezi kwa Rais John Magufuli.
Mdee anadaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) uliofanyika jana katika makao makuu ya chama hicho.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo Jumanne Julai 4 Hapi amesema kauli za Mdee kuhusu wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni, imemshtua yeye kama mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo.
Amesema ameamua kuchukua hatua hiyo hasa baada ya Mdee, alipomshushia kashfa hizo kiongozi wa nchi ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa nchi.
"Maneno yake ni ya kichochezi ambayo hayakubaliki, hayafai kutolewa na kiongozi kama yeye hivyo namuagiza kamanda amkamate Mdee amweke ndani kwa saa 48 ili ahojiwe yale yote aliyoyaongea ili afikishwe kwenye vyombo vya usalama,"amesema Hapi.

Chanzo: Mwananchi

No comments: