Advertisements

Saturday, December 30, 2017

ZIARA YA PROF NDALICHAKO MAGUFULI SEKONDARI WILAYA YA CHATO GEITA

Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia akiwa na viongozi wa Mkoa wa Geita wakati wa kukagua vyumba vya madarasa mwenye miwani kulia ni Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita.
Jengo la bwalo la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Magufuli lililopo Kata ya Bwanga Wilayani Chato ambalo limejengwa kupitia mpango wa lipa kulingana na matokeo (P4R).
Moja ya bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Magufuli lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 ambalo limetekelezwa kupitia P4R.
Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Magufuli, wakwanza kulia ni Mkuu wa shule hiyo na wapili kulia ni Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya Chato.
Mheshimiwa Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya ya Chato akizungumza na wananchi (awapo kwenye picha) wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu Wilayani Chato.
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Magufuli Sekondari.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bwanga wakati wa Ziara yake Magufuli Sekondari.
Bwana Exvery Nkanga kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Geita akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu Mkoa wa Geita kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia.

No comments: