Advertisements

Saturday, June 9, 2018

KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA MPANGO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA CHATEMBELEA ENEO LILILOTENGWA KWA AJILI YA MJI WA SERIKALI.

Makamu Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Joseph Kiraiya (watatu kutoka kushoto) akieleza jambo kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea eneo linalotarajiwa kujenga Mji wa Serikali Juni 7, 2018 Ihumwa Dodoma.
Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiweka nguzo ya umeme katika eneo la Ihumwa ambalo limetengwa kwa ajili ya mji wa serikali Dodoma
Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiweka nguzo ya umeme katika eneo la Ihumwa ambalo limetengwa kwa ajili ya mji wa serikali Dodoma.
Afisa Mipango Miji Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw.William Alfayo akiwaonesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea eneo hilo Juni 7, 2018.
Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Nigel Msangi akipata maelezo ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi kazi kutokana na ramani ya Mji wa Serikali walipotembelea kukagua eneo hilo Ihumwa, Dodoma.
Muonekano wa barabara itakayojengwa kwa kiwango cha lami ambayo itatumika katika Mji huo wa Serikali, Ihumwa Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakiangalia maeneo mbalimbali yaliyotengwa kulingana na ramani ya Mji mpya wa Serikali Ihuma Dodoma
Katibu wa Kikosi kazi cha kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akieleza jambo kwa wajumbe wa kikosi kazi hicho hiyo walipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali Ihumwa.
Eneo la Ihumwa ambapo Mji wa kiserikali unatarajia kujengwa hapo Jijini Dodoma
Katibu wa Kikosi kazi cha kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi kutoka TANROADS walipotembelea kukagua eneo hilo la Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

No comments: