Kundi la Waandishi wa Habari wakiwa katika boti maalumu kwa ajili ya safari ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Muonekano wa Mawe yaliyobebana ni miongoni mwa vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Sannane.
Muinekano wa lango la kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Baadhi ya Watalii wa ndani wakiwa katika Lango la kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiw acha Saanane kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi hiyo.
Baadhi ya Wageni wakipumzika katika moja ya maeneo yaliyopo katika Hifadhi hiyo.
Baadhi ya Vivutio vilivyomo ndani ya Hifadhi hiyo ,akiwemo ndege aina ya Tausi na Mnyama Simba.
Katika Hifadhi hiyo lipo ene maalum kwaa ajili ya kuweka kambi wakati wa kfanya shughuli ya utalii katika Hifadhi hiyo.
Eneo hili linajulikana kama Kona ya Siri "Scret Corner " iliyipo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saaanane ambayo imekuwa ikitumiwa na wanandoa kwa ajili ya kuombana msamaha.
Eneo hili linajulikana kama Jiwe la Kugusa "Touch Stone" ni moja la eneo ambalo watalii wa ndani wamekuwa wakitumia kupata Taswira .
Mti wenye muonekano wa mnyama Twiga "Giraffe Tree" ni kivutio kingine ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kilichopo jijini Mwanza.
Eneo hili limo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ambalo linajulikana kama jiwe la kuruka "Jump Stone" limekuwa ni kuvutio kwa wageni walitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kuchukua Taswira wakati wakiruka.
Mmoja waMhadhiri wa Chuo Kikuu cha St ,Agustine kilichopo jijini Mwanza,Judith Wanda akizungumza na wanahabri kuhusu kampeni inayozinduliwa leo ya kutangaza Vivutio vya Utalii katika jiji la Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ,Ikwabi Koroso akizungumza kuhusu kuanza kwa kampeni hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.
WADAU wa Utalii kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu katika jiji
la Mwanza leo wameanza kampeni ya siku
tatu ijulikanayo kama “Discover the Treasures of Mwanza” itakayoshirikisha
zaidi ya wanafunzi 800 waliojiunga na
vyuo vikuu mwaka huu.
Lengo la kampeni hii inayotarajia kufanyika katika Hifadhi
ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane linatajwa
kuwa ni kutoa fursa kwa wanafunzi hao wa elimu ya juu kutambua umuhimu wa
kutembelea rasilimali zilizopo nchini na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa
utalii wa ndani.
Akizungumzia tukio hili mmoja wa wajumbe wa kamati ya
maandalizi ya tukio hilo ambaye pia ni Mhadhiri
kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine(SAUT),Judith Wanda,anasema kampeni
hiyo inatarajiwa kuanza leo oktoba 26 hadi 28 mwaka huu.
Wanda amefafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wanafunzi hao
ambao ni wa mwaka wa kwanza watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu
kuhusu masuala ya uhifadhi na utalii wa ndani pamoja na namna bora ya kutangaza
vivutio vilivyopo nchini.
"Vyuo vinaanza udahili hivyo tumelenga wanafunzi wapya
wanaojiunga na elimu ya juu na tunatarajia kutumia fursa hiyo kuwafundisha
wanafunzi kutembelea vivutio na rasilimali zilizopo nchini kama njia ya
kujifunza na tunaamini hawa wataenda kuelimisha jamii umuhimu wa uhifadhi na
utalii wa ndani,"anasema na kuongeza
"Kampeni hii ya siku tatu imelenga kukutanisha
wanafunzi 800 na kila mwanafunzi atajigharamia kiasi cha Sh 8,800 kwa ajili ya
usafiri na shughuli nyingine hifadhini(Saanane),tulishawahi kufanya kampeni ya
kwanza na tulikuwa tukihusisha wanafunzi wa maeneo ya Mwanza,"
Awali Mkuu wa Idara ya Utalii katika hifadhi hiyo ya
Saanane,Ikwabi Koroso,anasema hali ya
utalii hifadhini humo imeimarika ambapo tangu ilipotangazwa Julai mwaka 2013
kuwa hifadhi ilikuwa na wastani wa wageni 4,000 kwa mwaka ila kwa sasa ni wastani
wa wageni 15,000 kwa mwaka.
"Hali ya utalii imezidi kuimarika,kati ya wageni hao
asilimia 96 ni wale wanaotoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na
mapato yanazidi kukua kulingana na idadi ya wageni hivyo tunatumai kupitia
kampeni hii itaongeza idadi ya watalii katika hifadhi yetu ambayo ni ndogo
kuliko hifadhi zote,"anasema
Kuhusu usalama kwa watalii,Mkuu huyo anawahakikishia watalii
kuwa usafiri huo wa kwenye maji uko salama na kuwa wanachukua tahadhari kubwa
ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa vyombo vya usafiri.
"Tunashirikiana na wadau wengine kutangaza utalii na
tunaamini kupitia kampeni hii tutaongeza idadi kubwa ya watalii katika hifadhi
yetu na maeneo mengine yenye vivutio katika ukanda huu,"
Naye Mkuu wa TTB
Kanda ya Ziwa,Gloria Mnihambo,anasema awali kabla ya kuanzishwa kwa
ofisi katika Kanda hiyo idadi ndogo ya watalii wa ndani walikuwa wakitembelea
Hifadhi na vivutio mbalimbali.
Anasema kuwa hivi sasa mwamko umekuwa mkubwa kwa watalii
ndani kutembelea vivutio hivyo baada ya kushirikiana na wadau wengine na kuwa
kupitia kampeni hiyo wataendelea kutangaza vivutio mbalimbaliili kuongeza idadi
hiyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment