JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MADINI
TAASISI YA JIOLOJIA NA
UTAFITI WA MADINI TANZANIA
S.L.P 903, DODOMA
Simu: +255 26 2323020
Nukushi: +255 26 2323020
Barua pepe: madini.do@gst.go.tz
TAARIFA KWA UMMA
WATALAAM WA TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA MADINI TANZANIA (GST) WAPOKEA TAARIFA YA MRADI WA JIOKEMIA KUTOKA KWA WATALAAM WA CHINA GEOLOGICAL SURVEY (CGS).Watalaam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania-GST) leo tarehe 10 Oktoba 2018 wakutana na watalaam kutoka taasisi ya jiolojia ya China (Geological Survey of China-CGS) kwa ajili ya uwasilishaji na upokeaji wa taarifa ya mradi wa Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo yaani (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika kwa ushirikiano baina ya serikali ya China na Tanzania
Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Bi.Yokbeth Myumbilwa amsema kuwa Utafiti huu umekusanya taarifa mbalimbali katika upande wa low density na high density ambapo kwa upande wa low density utafiti ulifanyika katika mkoa wa Mbeya na Songwe na high density ulifanyika kwa nchi nzima .
Akizungumzia juu ya faida zitokanazo na mradi huu wa ushirikiano , Myumbilwa alieleza baadhi ya malengo ya mradi kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa za jiokemia za nchini zitakazo ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini ,upangaji miji
,pamoja na taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbali mbali ndani ya sekta ya killimo na mazingira.
Faida nyingine ni upatikanaji wa taarifa hizi zitasaidia pia kuanisha aina mbalimbali za udongo kwa njia ya Ramani yaani (Geochemical Atlas Map of Tanzania).
Mnamo mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Geological Survey zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huu wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013mpaka 2018.
Akizungumza wakati wa kufunga hafla hiyo, Myumbilwa alishukuru kwa mafanikio makubwa ya mradi huo , pamoja ushirikiano mzuri uliokuwepo wakati wa utekelezaji wa mradi toka ulipoanza mwaka 2013.
Katika hafla hiyo ya upokeaji wa taarifa GST iliwakilishwa na watalaam kumi na mmoja na CGS iliwakilishwa watalaam sita ambao ni Sun Xiaoming ambaye ni mkurugenzi wa CGS, Sun Kai , Wang Huichu , TengXuegian , Li Janjian , Liu Xiaoyangi na Gong Kenghui.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA MADINI TANZANIA
GST
12 / 11 / 2018
No comments:
Post a Comment