ANGALIA LIVE NEWS
Monday, April 1, 2019
'YANGA SC KAMILI KUIFUTA NDANDA FC KESHO'
Jumla ya nyota 20 wa kikosi cha mabingwa wa kihistoria nchini, Yanga
Sc, kesho alfajiri kitaanza safari kueleka Mtwara tayari kwa mchezo wa
ligi dhidi ya wenyeji Ndanda Fc, mchezo uliopangwa kutimua vumbi, April
4 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Afisa habari Dismas Ten ameiambia Yanga Tv mapema leo kuwa Nahodha
Ibrahim Ajib ataendelea kukosekana kikosini kupisha majeraha madogo
aliyo nayo huku Juma abdul akirejea kikosini baada ya kupona majeraha
yake.
"Ibrahim Ajib bado tutaendelea kumkosa kikosini kutokana na majeraha ya
mguu,lakinijambo jema ni kwamba Juma Abdul amerejea kikosini na atakuwa
sehemu ya msafara wa kikosi chetu,mchezo utakuwa mgumu lakini maandalizi
tuliyoyafanya yanatosha kutupa matokeo mazuri".
Zaidi ingia www.yangasc.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment