Advertisements

Tuesday, June 2, 2020

ZIARA YA MHE. WAZIRI MKUU MKOANI TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga, akiwa katika ziara ya siku moja, kukacgua maendeleo ya zao la mkonge, mkoani Tanga, Juni, 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa Jengo la Mamlaka ya Mkonge, akiwa katika ziara ya siku moja, kukagua maendeleo ya zao la mkonge, mkoani Tanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Mamlaka ya Mkonge, akiwa katika ziara ya siku moja, kukagua maendeleo ya zao la mkonge, mkoani Tanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mti wa mkonge uliopandwa nje ya Jengo la Mamlaka ya Mkonge Mkoani Tanga, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Mamlaka hiyo, kutoka kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omar Mgumba, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania Saad Kambona, akiwa katika ziara ya siku moja ya Mkoa huo, kukagua maendeleo ya zao la mkonge,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omar Mgumba, baada ya kukagua shamba katika kituo cha utafiti wa zao la mkonge TARI Mlingano, akiwa katika ziara ya siku moja ya Mkoa huo, kukagua maendeleo ya zao la mkonge
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi kituo cha utafiti wa zao la mkonge TARI Mlingano, akiwa katika ziara ya siku moja ya Mkoa huo, kukagua maendeleo ya zao la mkonge
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasili katika Jengo la Mamlaka ya Mkonge, Mkoani Tanga kabla ya kulizindua rasmi, akiwa katika ziara ya siku moja ya Mkoa huo, kukagua maendeleo ya zao la mkonge, Juni, 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: