ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 8, 2022

NYUMBANI KWA WAFIWA FREDERICK, MARYLAND

Hashim kutoka Massachusetts akijumuika pamoja na familia ya Akida nyumbani kwa wafiwa Frederick, Maryland. Maziko ya Seif Akida yatafanyika siku ya Jumamtano Feb 9, 2022 baada ya sala ya adhuhuri, Maziko yatafanyika katika makaburi ya Al Firdaus Memorial Gardens anuani 3845 Design Rd, Frederick, MD 21703 saa 7 mchana (1pm).
Salim Akida (kushoto) mdogo wa marehemu akitoa maelekezo kwa njia ya simu, kulia ni NY Ebra.
Mwenye fulana nyeupe ni Bilal kutoka New York akikorofisha maakuli jikoni.
Bilal akiendelea na menyu yake.
Kutoka kushoto ni Salim, Juma na Hashim katika picha ya pamoja.
Bilal akiwakaribisha supu wakeni waliojumuika pamoja na wafiwa.

No comments: