ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 6, 2026

TAMASHA LA SANJO YA BUSIYA 2026 LAZINDULIWA RASMI, WATANZANIA WAHIMIZWA UPENDO NA AMANI

 


Na. Matukio Daima Media App, Kishapu, Shinyanga.


MTEMI wa Busiya Ntemi Makwaia wa iii amezindua rasmi tamasha la Sanjo ya Busiya  maarufu kama  Sabasaba (7-7) huku Wananchi wakihimizwa upendo na Amani.

Uzinduzi huo umefanyika jioni ya Julai 5,2026  umefanyika katika eneo la Ikulu ya Busiya  na Mtemi wa Busiya Ntemi Makwaia wa iii pamoja na Machifu wengine kutoka meeneo mbalimbali ikiwemo: Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mara, Mwanza, Ruvuma, Mkoa mwenyeji wa Shinyanga na Taifa la  Afrika Kusini, ambao kwa pamoja walipata pia kutoa neno la Shukrani.

Awali, Ntemi Makwaia iii alishuhudia matukio mbalimbali ya tamasha hilo ikiwemo ngoma za asili kutoka Jamii ya Wasukuma.



Mtemi wa Busiya Ntemi Makwaia wa iii  akivikwa mavazi maalum ya kiutawala


Aidha, amewatakia Wananchi kuendelea kupendana na kudumisha amani sambamba na kuendeleza utamaduni.

Tamasha hilo limekuwa likikusanya umati mkubwa kutoka ndani na nje ya Nchi wakifika kwa wingi kushuhudia matukio ya Ngoma za asili na kila za Jamii ya Wasukuma kutoka Busiya na maeneo jirani.

Ambapo pia Wananchi wanapata fursa za  huduma za afya ikiwemo kupimwa Afya zao bure kutoka kwa Watalaam na Madaktari wa Afya Check, pamoja na Hospitali ya jirani.

Tamasha hilo linatarajiwa kufika kilele chake Julai 7, 2026 ambapo shughuli za Ngoma , vyakula vya asili na manunuzi ya bidhaa mbalimbali zinaendelea kunogesha tamasha hilo kila mwaka tokea kuanzishwa kwake miaka 16 iliyopita.



















No comments: