Thursday, February 11, 2010

Rufaa ya Babu Seya, wanawe waachiwa

Mwanamuziki Nguza Viking (kushoto) na wanawe, kutoka kushoto Papii Nguza, Nguza Mbangu, na Francis Nguza wakiwa katika Mahakama ya Rufani Tanzania, Dar es Salaam kusomewa hukumu ya rufaa yao kupinga adhabu ya kifungo cha maisha jela. Mbangu na Francis wameachiwa huru
MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania imeridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa mwanamuziki maarufu, Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza.

Mahakama hiyo imewaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.

Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Neema Chusi, amesoma hukumu hiyo leo kwa saa mbili jijini Dar es Salaam.

Baada ya hukumu hiyo, mahakama ilikuwa kama eneo la msiba kwa kuwa Babu Seya na wanawe walibubujikwa machozi, na ndugu na jamaa zao walilia kwa sauti...chanzo Habari Leo

1 comment:

Anonymous said...

Mimi naona wameonewa sana,ingawaje mimi pia na mwamke na nina watoto wa kike! je kuna uhahidi wowote ule ndio maana huku ugaibuni kuna DNA,mimi siamini kabisa kama wamefanya hivyo!na hao walioachiwa wafuate taratibu za sheria wawashtaki hao watu wanaona wanastahili kushtakiwa,yaani hapa kwetu Tanzania hakuna haki kabisa!!! inashangaza eti nchi inayojiita yenye Amani inafanya upuuzi huo,labda kwasababu hakimu pia alikuwa mwanamke(nimetoa mfano tu)naomba kwa mtu yoyote anayejua information yoyote ya haki za binadamu na utetezi wake popote duniani aweke hapa kwenye hii blog ili tuweze kuwasaidia hawa wenzetu,wameona mzee seya na paapi kocha wana kipaji cha mziki ndio maana wamewarudisha ndani wale ambao sio sana wamewaachia,yaani huo ni wivu,roho mbaya na uchawi!tafadhalini sana watanzania wenzetu tusaidiane kwa hilo,na nawaomba nitumieni information za haki duniani tafadhali.