Sunday, February 14, 2010

Raila awasimamisha kazi mawaziri


Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amewasimamisha kazi mawaziri wawili ili kutoa nafasi ya uchunguzi kuhusu kashfa mbili za ufisadi.
Kulingana na waziri mkuu, mawaziri hao, William Ruto na Professa Sam Ongeri wamesimamishwa kazi kwa kipindi cha miezi mitatu.
Bw Odinga amesema amechukua hatua hiyo kwa kuwa ripoti mbili za uchunguzi uliofanywa na mashirika mawili tofauti zimetoa sababu za kutosha kuonyesha mawaziri hao wanastahili kuchunguzwa zaidi kuhusiana na kashfa za ufisadi.
Awali rais Mwai Kibaki aliwasimamisha kazi maafisa wanane wakuu serikalini kuhusiana na kashfa hizo zinazohusu mahindi yaliyouziwa matajiri kwa njia ya ufisadi , na pia ubadhirifu wa mamilioni ya pesa zilizokusudiwa kugharamia elimu ya bure nchini Kenya.

No comments: