Wednesday, February 10, 2010

Spika Sitta ashtuka kuitwa Madam!

Katika hali inayoonesha kuwa kindumbwendumbwe cha homa ya uchaguzi kinaendelea kupanda siku hadi siku,asubuhi hii mjengoni (Bungeni dodoma)...mbunge mmoja katuma kimemo kwa spika wa bunge la jamhuri ya watu wapole..akiwa amekiaddress kwa jina la Madam Speaker.

Kitendo hicho kilimshtua spika wa bunge ambapo aliamka huku akicheka na kuwaomba wabunge wapunguze homa ya uchaguzi..."waheshimiwa wabunge naombeni muache homa ya uchaguzi..mbona muda badooo..muda sio mrefu nimepokea kimemo flani hapa kimeaddresiwa kwangu kwa jina la madam speaker" kitendo kilicholitikisa bunge zima kwa kicheko takriban dk 3 na usheee

No comments: