Mtakwimu wa ICAC, Bw. Andrei Guitchounts, akitoa mlinganisho wa matumizi
ya pamba kwa miaka 2 iliyopita (2010/11, 2011/12) na matarajio kwa mwaka
2012/13 na wajumbe wakifuatilia.
Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Balozi
Mwanaidi Maajar.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar(aliyesimama), akiwakaribisha wajumbe wa Mkutano huo Tanzania House kabla
ya mkutano kuanza. Waliokaa pembeni mwake ni Mwenyekiti wa Kamati, Bibi
Lily Letawo Munanka na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Terry Townsend.
Mwenyekiti, Bibi Lily L. Munanka akiendesha mkutano huo na wajumbe
wakifuatilia. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa ICAC, Bw. Terry
Townsend
Mkutano wa 520 wa Kamati ya Kimataifa ya Ushauri Kuhusu Pamba
(International Cotton Advisory Committee) umefanyika Ubalozi wa Tanzania
Washington DC tarehe 20 Septemba, 2012, ambapo Tanzania ni Mwenyekiti kwa
mwaka 2011/2012.
Mwakilishi wa Tanzania kwenye Kamati hiyo ni Mkuu wa Utawala na Fedha Bibi
Lily Letawo Munanka ambaye sasa ndio Mwenyekiti baada ya kuwa Makamu wa
Kwanza wa Mwenyekiti 2010/2011 na Makamu wa Pili wa Mwenyekiti 2009/2010.
ICAC ilianzishwa mwaka 1939 mjini Washington, DC kwa lengo la kusaidia
nchi wanachama kuendeleza zao la pamba na kulipa nafasi katika uchumi wa
dunia kwa ujumla.
Aidha Kamati hiyo hutoa taarifa mbalimbali za uzalishaji, biashara na
matumizi ya zao la pamba na mabadiliko ya soko duniani ambayo yanaweza
kusababishwa na mambo hayo matatu. Tanzania (Tanganyika) ilijiunga mwaka
1962 na ni miongoni mwa nchi wanachama 41.
ICAC pia ni jukwaa la nchi wanachama kuzungumzia masuala mbalimbali ya
kimataifa kuhusu pamba ambapo Tanzania pamoja na nchi nyingine
zinazoendelea hutetea maslahi yao.

No comments:
Post a Comment