Filamu Mpya Ya My Man Sehemu ya 2 inatarajiwa kuingia Sokoni muda si mrefu kutokana na kumalizika kwa kazi nzima ya utengenezaji wake.
Filamu hii ya kitanzania ambayo story yake imeandikwa na Kijana Geric Kimaro anayesomea Shahada ya Kwanza ya Filamu katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akiwa mwanafunzi wa Mwaka wa 2 Chuo Hapo.
Akiongea na Mtandao wa LUKAZA BLOG amesema " Mashabiki wa filamu za kitanzania wakae Mkao wa Kula kwasababu kwanza hawataboreka kutokana na waigizaji wake ni Vijana wanaosomea fani ya Filamu katika ngazi ya Shahada ya Kwanza ambao wana vipaji na ujuzi pia katika tasnia ya filamu nchini lakini pia Katika filamu hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya BORNAGAIN na kumshirikisha Nguli wa filamu za Bongo Mwenye Swaga za Uchungaji, Pastor Myamba."
Mbali na Kumshirikisha Pastor Myamba amesema kuwa katika filamu hiyo kuna sura mpya nyingi ambazo ni vipaji na zao kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambapo wengi wao ni wanafunzi wanaosomea Shahada ya Kwanza ya Filamu,Na amefanya hivi kuonyesha na Kutambulisha vipaji ambavyo badi vipo Shuleni.
Alimalizia kwa Kusema kuwa Filamu hii sio ya Kukosa kwasababu humo ndani ni kuna vitu vipya ambavyo havijawahi kuonekana katika filamu za bongo, Kwahiyo Usikose nakala Yako
No comments:
Post a Comment