Walinzi
wa mwambao kutoka shirika la majeshi ya muungano ya NATO wanawatafuta
manusura wa boti iliyozama ufuoni mwa kisiwa cha Lampedusa ambapo mtu
mmoja alifariki na wengine wengi bado hawajulikani waliko.
Manusura wengine 56 wakiwemo wanawake wajawazito wameokolewa kutoka kwenye boti hiyo iliyozama mapema leo asubuhi.
Kisiwa
cha Lampedusa ambacho kiko umbali wa kilomita 120 kutoka Tunisia, ni
eneo ambalo hutumiwa na wahamiaji wengi haramu wa kiafrika kuingia
barani Ulaya kwa sababu ya ukaribu wake kwa bara hilo.
Maafisa
wanasema kuwa idadi ya watu waliokuwa kwenye boti hiyo heunda ikawa
zaidi ya miamoja ikilinganishwa na idadi iliyokuwa imeripotiwa awali.
Baadhi
ya manusura waliokolea kutoka baharini na wengine walikuwa kwenye
sehemu ya kisiwa hicho ambako hakuishi watu.Msemaji wa walinzi wa NATO,
alinukuliwa akisema watu 56 wamepatikana wote raia wa Tunisia.
Mnamo
siku ya Alhamisi, watu 56 walizama wengi wao wakiwa watoto baada ya
boti yao kuzama Magharibi mwa pwani ya Uturuki. Wengine 45 waliokuwa
kwenye boti hiyo walinusurika.Wahamiaji hao haramu walikuwa wairaqi,
raia wa Syria na wapalestina wakikimbilia barani Ulaya.
Kulingana
na shirika la kimataifa la Amnesty International, mnamo mwaka 2011,
takriban watu 1,500 walizama katika bahari ya Mediterranea wakiwa njiani
kuelekea barani Ulaya.Wengi walikuwa wanatoroka vurugu nchini Tunisia
na Libya,wakati wa harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
1 comment:
mungu awasaidiye aisee, ndo maisha wote tunatafuta hakuna aliye zaliwa amekuja nacho,so mungu awasaidia because namkumbuka bro wangu alizamia meli toka ana umri wa miaka 15 mungu awasaidiye wasitiwe matatani na kauli hizi za kuchepua chepua noma kweli eti wahamiaji haramu nani aliye halali?
kipi kilicho cha halali katika dunia hii, tunaishi marekani kulipa tax siyo halali ukifanya uchabuzi utalijua hili lakini tunalipiswa kwa vile mayahudi ndo wanachotaka ndo nchi yao hivi sasa wao ndo wanao hozi hii nchi,
amkeni wabongo wenzangu
shukuru mungu tu una ajira na riziki inaingia mdomoni other wise vyote vya haramu tu na uonevu
Post a Comment