Tuesday, March 12, 2013

Mauaji ya albino yaichafua Tanzania


Mwenyekiti wa Chama Cha Albino Tanzania(CCMT), Ernesti Kimaya akijibu swali la waandishi wa habari wakati alipozungumzia uchaguzi mkuu ujao wa chama hicho jijini Dar es Salaam. Kulia ni mweka hazina, Abdillah Omar. Picha na Zacharia Osanga.


Mpango wa Afrika wa Kutathmini Utawala Bora (APRM), umebaini kwamba rushwa na ukiukaji wa haki za binadamu ni tatizo kubwa nchini linalohitaji kufanyiwa kazi ili kuimarisha utawala bora.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba, licha ya Tanzania kuonyesha mafanikio katika utawala bora, bado maeneo hayo yanahitaji nguvu za ziada.
Mahadhi alisema hayo wakati wa kuadhimisha Siku ya APRM ikiwa ni miaka 10 tangu ilipoanzishwa.
“Ripoti ya APRM iliwasilishwa na Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa wakuu wa nchi za Kiafrika na kusifiwa sana,” alisema.
Alisema kuna mambo machache yalijitokeza na yanayoharibu jina la Tanzania na watu wake.
Alisema kukithiri kwa rushwa ni sehemu ambayo ilitia doa katika ripoti hiyo na kwamba inahitaji kufanyiwa kazi.
“Tunahitaji kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Tume ya Maadili ya Viongozi ili kuondokana na kasoro hizo,” alisema Mahadhi.
Aidha alisema eneo la haki za binadamu nalo lilitia doa katika ripoti hiyo hasa mauaji ya walemavu wa ngozi (albino).
Mwananchi
ANGALIA DOCUMENTARY VIDEO YA MAUAJI YA ALBINO TANZANIA kwa kubofya read more 

Africa Investigates : The spell of the Albino


In this episode of Africa Investigates, Tanzanian journalist Richard Mgamba, albino community representative, Isaack Timothy, and Ghanaian investigative journalist Anas Aremeyaw Anas set out to discover what lies behind the attacks against albinos.

No comments: