Thursday, August 20, 2015

NEC KUTANAGZA MATOKEO YA URAIS NDANI YA SIKU TANO.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva 

Tume ya taifa ya uchaguzi imewatoa hofu watanzania kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu imejiimarisha kimfumo wa kielektronic kuhakikisha matokeo yote yanayopatikana yanatangazwa ndani ya kipindi kifupi huku ikiahadi kutangaza matokeo ya urais ndani ya siku tano.
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi inasema katika kipindi hiki hakutakuwa na dosari zozote za kimfumo hasa taarifa za wagombea huku ikijinasibu kuwa kupitia mfumo wake mpya wa kupokea, kuhesabu na kujumlisha matokeo ambao uko kielektronic hakutakuwa na ucheleweshaji wa kutangaza matokeo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva anasema ni vema vyama vikafuata kanuni na sheria za uchaguzi katika kampeni kwani kushindwa kufanya hivyo nikuilazimisha tume kuchukua hatua kali za kisheria.


Katika mahojiano yao na ITV muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa mkutano baina ya viongozi wa dini na tume ya taifa ya uchaguzi baadhi ya viongozi hao wa dini pamoja namasuala mengine walikuwa na haya ya kuzungumza.

Kuelekea Agast 22 mwaka huu ambapo ndio filimbi ya kaushia kuanza kampeni za mwaka itakapopulizwa, NEC bado inasisitiza kwa vyama, wafuasi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya nchi.

CHANZO: ITV TANZANIA

7 comments:

Anonymous said...

Tume ya uchaguzi nayo kuweni na usawa. Tunaona yanayofanyika kwenye vituo vya utangazaji Televisheni na magazeti yameshaonywa na wanaonekana kubeba tu habari za chama tawala CCM inayofifia. Hii sio haki wizara inayohusika haiwezi kuwa upande mmoja na mseme haki ipo. Huu ni ufisadi wa hali ya juu. Hebu iachwe mara moja. Kamati iloyombeba Makyembe hebu iueleze umma alipokuwa wizara aliyotoka alikamata madawa ya kulevya kwa wingi pale JK uwanjabwa ndege ikaisjia hewani hatukuambiwa ninya nani nanhatua gani zilichukuliwa. Kwa kulindwa akahamishwa wizara!! Yaani kuwalinda wana CCM waliohusika ndani ya serikali. Waziri Sita aliyeharibu katiba kapewa wizara jiyo. Pembe na vipusa kadhaa zimepitishwa hapo majuzi na wamekaa kimya pamoja na waziri Lazaro kweli Tanzania tuna viongozi jamani au watafunaji??

Anonymous said...

Hakuna kitu ambacho hiki chombo kimefanikiwa kufanya vema. Itawezekanaje kwa matokeo?

Anonymous said...

Tunashukuru kwa kauli nzuri lakini basi na muwe na haki msielemee upande mmoja na kuchakachua kwa magoli ya mkono. Tumeshaanza kuyaona tangu mwanzo huu..

Anonymous said...

Ni electronics gani ambayo inachukua siku tano? Electronic means instantly.. Ni kama kutuma emails, haichukui siku tano. Lubuva usijenge mazingira ya kuleta umwagaji damu Tanzania

Anonymous said...

Tunaiomba na kuishauri tume ya uchaguzi hili mnalolileta la ndani ya siku TANO (5) liishe yaani mara moja na wataalamu waangalizi wa nje msikubaliane na hili kama tumeingia kwenye mtindo wa electronic una maana kura zinapigwa na zinaendelea kuhesabika na kutoa matokeo ya awali kila baada ya muda usiozidi lisaa limoja ! hivyo kwa misingi hii kura zinapigw ana kumalizika jioni saa mbili. Hakuna kulala na umeme uwepo hata kama ni generator ifanye kazi na matoke yaanze kutangazwa ifikapo asubuhi kwenye vyombo vya habari ikiwemo TV ZOTE NA BREAKING NEWS ZA MARA KWA MARA. Huo ndio uzalendo na demokrasia sasa hizo siku tano inamaana mnaenda kupiga kura mpya zaidi. Hebu tuache kutawaliwa na miundo ya 1961 tulipopata uhuru!! Tunakuomba kama hutaweza kuandaa utangazaji wa haraka uombe kuacha hiyo nafasi ili wataalamu wakae hapo. Asante mheshimiwa.

kidoo said...

Tena futa kauli za baada ya Siku tano mnataka kutuibia kura zetu au mjue watanzania hasav sisi wakina mama tumemka sasa kama kuingia barabarani na sisi tutaingia ole wenu NEC mlete upumbavu mbele yetu msije sema hatujawaonya mapems

Anonymous said...

Siku tano mbona nyingi sana!