Thursday, August 20, 2015

NYALANDU ACHUKUA FOMU YA NEC KUWANIA UBUNGE

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akichukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Singida, Faridda Mwasumilwe katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo, juzi. 
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akipokewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kinyagigi katika Jimbo la Singida Kaskazini wakati alipokwenda kuzungumza nao, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akicheza na makada wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Kinyagigi muda mfupi baada ya kuchukua fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida.
WANANCHI wa Kijiji cha Kinyagigi katika Jimbo la Singida Kaskazini, wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya kuchukua fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati), ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida, muda mfupi baada ya kuchukua fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kinyagigi, jimboni humo juzi.

2 comments:

Anonymous said...

Laana itakushukia wewe na wote wanaokuunga mkono ndani ya CCM. Kwa wote mnaoipanda Tanzania yetu tafadhali ongeleeni hili swala kwani sio la CCM au UKAWA bali ni la watanzania wote. Muombeni atoe maelezo kuhusu pembe za ndovu kilo 262 zilizokamatwa Zurich airport zikitokea Tanzania? Unaongelea zaidi ya tembo hamsini wameuwawa ili kupata hiki kiwango. Au ndio utanzania wenyewe huu kwamba sasa una hela ya kuwalipa bodaboda na kufuturisha.

kidoo said...

Kweli mwenzangu tujiulize hao tembo wamewaua ili iweje pia wanasingida niwapumbavu sana watamchugua mimi sioni chochote kipya katika mkoa wa singida na niwaziri hakuna chochote alichokifanya singida na sio yeye tu hata wabunge wangu wa ukawa hawajafanya kitu singida kamji kaovyo mno mno kanashindwa ata na wilaya ya nzega na kahama