Advertisements

Tuesday, April 18, 2017

KASHFA ZITO HOSPITALI YA TEMEKE

Asma Juma na mumewe Aboubakar Pazi wakiwa na
By James Magai na Jackline Masinde, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Utata umeibuka baada ya mkazi wa Mbande jijini Dar es Salaam, kuishutumu Hospitali ya Wilaya ya Temeke kumuimbia mtoto mmoja, baada ya kujifungua pacha.

Mwanamke huyo, Asma Juma alisema kabla ya kwenda kupewa rufaa ya kujifungua katika hospitali hiyo, alipima kipimo cha ‘ultrasound’ na kuthibitishiwa kuwa ana mapacha.

Asma alisema awali alikuwa akipata huduma za kliniki katika Zahanati ya Serikali ya Mbande, lakini alikuwa amefanya vipimo vya ‘Ultrasound’ katika Zahanati ya binafsi ya Huruma iliyopo Mbande mara mbili na kuthibitishiwa kuwa ana pacha.

“Wakati napelekwa chumba cha upasuaji nilikuwa sina kichaa cha uzazi, siumwi uchungu, siumwi kichwa, siyo kipofu, siyo kiziwi, nasikia kwa masikio yangu na kumbukumbu zote nimezihifadhi kwenye kichwa changu. Ninachotaka ni mtoto wangu,” alisema Asma.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo alikiri kuwapo kwa tuhuma hizo na kusema tayari zinafanyiwa kazi na uongozi.

No comments: