Advertisements

Tuesday, March 9, 2021

AFCON chini ya miaka 17 yafutwa, Serengeti kurejea

By Thomas Ng'itu, Mwanaspoti

SHIRIKISHO la soka barani Africa (CAF) limefuta fainali za AFCON chini ya miaka 17 zilizokuwa zinaanza Machi 13, 2021 nchini Morocco.

Maamuzi ya fainali hizo kuvunjwa yalifanyika baada ya kikao cha dharula kufanyika jana Jumatatu nchini Morocco na kumalizika jioni.

Kikao hiko kilichambua kuhusu ugonjwa wa covid 19 katika nchi ya Morocco na ndipo walipoamua kufuta mashindano hayo mara moja.

Wakati mashindano hayo yakifutwa timu sita kati ya 12 zilizofuzu zilikuwa zimeshafika ambazo ni Tanzania, Zambia, Uganda,Senegal na Ivory Coasta.

CAF wiki iliyopita walifanikiwa kumaliza salama fainali za AFCON chini ya miaka 20 zilizofanyika nchini Mauritania huku Ghana wakiibuka mabingwa.

No comments: