Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba (kulia), akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran (kushoto) aliyemtebelea ofisini kwake wiki iliyopita. Anayefuata kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti -GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ushirika (Afrika), Simon Shayo pamoja na viongozi wengine wa GGML. Wakati wanaofuata kulia ni baadhi ya maofisa wa wizara ya fedha.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran aliyemtebelea ofisini kwake wiki iliyopita. Anayefuata kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti -GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ushirika (Afrika), Simon Shayo pamoja na viongozi wengine wa GGML. Wakati wanaofuata kulia ni baadhi ya maofisa wa wizara ya fedha.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba amesema mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Serikali na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) yamechangia kukuza uchumi wa Taifa hususan kwenye makusanyo mazuri ya kodi, ajira na manunuzi ya bidhaa na huduma kutoka ndani ya nchi.
Pia amesema GGML ambao wamekuwa wadau wazuri kwenye sekta ya madini pamoja na ushirikiano mzuri unaotolewa kwa wizara ya madini umeendelea kukuza sekta hiyo ya madini na kutoa mchango mkubwa kwa jamii na Taifa.
Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dodoma alipokuwa anazungumza na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki mgodi huo wa Geita Gold Mine-GGM), Gillian Doran.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Mwigulu amesema; “Tumekuwa na mahusiano mazuri sana na GGML kama wizara ya fedha hususani katika masuala ya kikodi na kiuchumi.
“GGML wamekuwa wadau muhimu sana wa masuala ya kodi na masuala ya kukuza uchumi wa nchi yetu pia wamekuwa mahusiano mazuri na wizara ya kisekta (madini) kwa kuwa moja ya mgodi wa mfano ambao una ushirikiano mkubwa na wizara ya kisekta na wizara nyingine kama sisi,” amesema Dk. Mwigulu.
Aidha, ameseema GGML umekuwa moja ya mgodi wa mfano wenye mahusiano mazuri na jamii mgodi ulipo kwa kutekeleza ipasavyo mpango wa uwajibika wa kampuni kwa jamii (CSR).
Pamoja na mambo mambo mengine ametoa mwito kwa kampuni hiyo kutumia viwanda vya kuchenjua dhahabu kwa njia ya kusafisha iliyopo nchini ili kuendelea kukuza uchumi wa Taifa.
Aidha, katika majadiliano hayo Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran aliyemtembelea Dk. Mwigulu akiwa na timu ya uongozi wa kampuni hiyo, alimweleza waziri huyo kuhusu mipango ya muda mrefu ya AngloGold Ashanti kwa Tanzania.
Amemshukuru Dk. Mwigulu kwa kutambua mchango wa GGML ambayo imeendelea kusalia kuwa mlipakodi bora zaidi katika tasnia ya uziduaji nchini.
No comments:
Post a Comment