Friday, February 2, 2024

RUFAA YA MARIA NGODA ALIYEFUNGWA MIAKA 22 KWA KUKUTWA NA NYAMA YA SWALA YASIKILIZWA



HAKAMA Kuu ya Mkoa wa Iringa chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta jana Februari 1, 2024 imesikiliza kesi ya Rufaa Namba 84101/2023 kati ya Maria Ngoda dhidi ya Jamuhuri.

Akiongoza jopo la Mawakili upande wa mkata rufaa Wakili Moses Ambwindile amesema leo wametetea sababu zao za Rufaa 14 mbele ya Jaji Mfawidhi.

Aidha Jaji Mgetta iliahirisha shauri hilo mpaka Leo tarehe 2 Februari 2024.

Mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) alihukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3,2023.

No comments: