Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Ester John ambaye alimchangia uloto mdogo wake Elisha John katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Kareem Mjata ambaye amepandikizwa uloto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024. Kareem Mjata amechangiwa uloto na Ndugu yake Miriam Mjata
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipinga na Deus Mwita ambaye amelazwa katika Kitengo cha upandikizaji uloto kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024. Mtoto huyo amemuahidi Rais Samia kuwa atasoma kwa bidii mara baada ya kupona ugonjwa wa Selimundu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Laurean Kanaganwa ambaye bado hajapandikizwa uloto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024
No comments:
Post a Comment