ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 23, 2025

UFAFANUZI TAARIFA INAYOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII INAYOHUSU GARI LA POLISI KUBEBA WANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA

 



TANZANIA YAMNADI PROF. JANABI NAFASI YA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA


Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (Mb.) akimnadi mgombea Prof. Janabi nafasi ya Mkurugenzi wa Who Kanda ya Afrika.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemtangaza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Yakub Janabi kuwa Mgombea wa Nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.

Akibainisha sifa na uwezo binafsi wa mgombea huyo katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (Mb.) amesema kuwa Prof. Janab ni mgombea sahihi mwenye uwezo wa kazi na kufanya mageuzi pamoja na maboresho katika sekta ya afya.

MKUCHIKA ATANGAZA KUNG'ATUKA UBUNGE



Na Regina Ndumbaro - Newala.
Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini, Mheshimiwa George Mkuchika, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalum, ametangaza kutogombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Tangazo hilo amelitoa katika mkutano maalum wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika ukumbi wa Nawema, Newala Mjini.

Akizungumza katika mkutano huo, amesema kuwa amehudumu katika siasa na utumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 50 na sasa ni wakati wa kuwaachia vijana waongoze. Mheshimiwa Mkuchika ameeleza kuwa safari yake ya uongozi ilianza baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1973.

Tangu mwaka 1983, alihudumu kama Mkuu wa Wilaya katika maeneo mbalimbali kabla ya kuteuliwa na Hayati Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkuu wa Mkoa, nafasi aliyoitumikia kwa miaka minane.

Mwaka 2005, wananchi wa Newala walimsihi kuwania ubunge, na alikubali kuacha nafasi ya ukuu wa mkoa ili kuwatumikia wananchi wa Newala Mjini.

MWALIMU JACOB MBUNDA AIBUKA MSHINDI WA UENYEKITI CWT NAMTUMBO


Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ibula Ngonyani (kulia),akipokea cheti maalum baada ya kuibuka mshindi wa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania kitengo cha Wanawake uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Samia Suluhu Hassan.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania(CWT)Sabina Lipukila kushoto akikabidhi cheti kwa Mwalimu Amodzize Kinyamagoha baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya Ujumbe kwenye uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kitengo cha Wanawake.

WARSHA YA USALAMA WA ANGA AFRIKA YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM



 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi, ameifunga rasmi warsha ya kikanda kuhusu usalama wa anga iliyoshirikisha washiriki 72 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika. Warsha hiyo ya siku tano, iliyoanza Machi 17 na kuhitimishwa Machi 21, 2025, jijini Dar es Salaam, ililenga kujadili na kuimarisha mikakati ya kuboresha usalama wa anga, ufanisi wa usambazaji, na uendelevu wa sekta hiyo kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa na miongozo ya kimataifa.

Akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo, Bw. Msangi alisisitiza kuwa mjadala wa washiriki umewezesha kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya usafiri wa anga barani Afrika na njia bora za kuzitatua.

“Katika warsha hii, washiriki wamejadili changamoto zinazozikabili nchi zao na taasisi zao za usafiri wa anga, hususan kuhusu mifumo ya mawasiliano ya usafiri wa anga. Kupitia majadiliano haya, tumepata fursa ya kujadili namna bora ya kushughulikia changamoto hizi kwa pamoja, kwa sababu hakuna nchi inayoweza kufanya kazi peke yake,” alisema Msangi.

Aliongeza kuwa washiriki wa warsha wameahidi kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha sekta ya anga inakuwa salama na yenye ufanisi zaidi.

NBAA YATOA ELIMU SHULE YA SEKONDARI YA NGUVUMALI MKOANI TANGA



Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nguvumali iliyopo mkoani Tanga.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari mkoani Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya Uhasibu.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwahamasisha wanafunzi walioko shuleni hasa shule za Sekondari kupenda na kusoma masomo ya Uhasibu ili waweze kwa wanataaluma wa fani hiyo.

Pia amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili aweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Saturday, March 22, 2025

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE HARAMBEE


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini , Dkt. Frederick Shoo, kwenye Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa hilo iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini , Dkt. Frederick Shoo (kushoto) wakinadi chupa za kuhifadhia vimiminika katika Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa hilo iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo iliyofanyia kwenye hoteli ya Serena jijini Dar eś salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akinadi saa iliyouzwa kwa sh. Mimilioni 4.4 katika Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

CHIFU WA MBEYA ROCKETI MASOKO MWANSHINGA AKEMEA WANAPANGA KUZUIA WANANCH...

CHIFU WA MBEYA ROCKETI MASOKO MWANSHINGA AKEMEA WANAPANGA KUZUIA

 WANANCHI KUJITOKEZA KWENYE UCHAGUZI




Chifu wa Mkoa wa Mbeya, Rocketi Masoko Mwanshinga, amewataka wananchi wote wa mkoa huo

 kutumia haki yao ya kikatiba kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.



Chifu Mwanshinga amekemea vikali wale wote wanaotaka kuwazuia wananchi kushiriki katika mchakato

 wa uchaguzi, akisema Mungu atawapa usingizi na hawataweza kuzuia uchaguzi kufanyika.



Amesisitiza kuwa kila raia ana haki ya kupiga kura na kupigiwa kura bila hofu wala vizuizi vyovyote. A

idha, Chifu Mwanshinga amemuombea Rais Samia Suluhu  Hassan apate ushindi wa kishindo, akisema kuwa uongozi wake umekuwa wa neema kwa Watanzania.




Amewataka wakazi wa Mbeya kuungana kwa mshikamano na kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kidemokrasia ili kuchagua viongozi watakaosukuma mbele maendeleo ya Tanzania.


Friday, March 21, 2025

ARUSHA FOOD SYSTEMS YOUTH LEADERS WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA CHAKULA MASHULENI



Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula Mashuleni Arusha Food Systems Youth Leaders wametembelea shule ya sekondari Ungalimited na kutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na walimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwa ajili ya kuwa na mifumo endelevu ya chakula ikiwemo kupanda miti ya matunda.

Viongozi vijana wa mifumo ya chakula Arusha, wanafunzi pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari Ungalimited wameweza kupanda miti ya matunda katika shule hiyo takribani miti 50 ambayo ni mipapai 10, miembe 10, mipera 10, michungwa 10 na matopetope 10.
Pamoja na kupandaji miti vijana hao walifanikiwa kuzungumza na wanafunzi kuhusu umuhimu wa elimu katika maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla pamoja na faida za kupanda miti ya matunda kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora kwa kizazi cha sasa na cha baadae.

RIPOTI YA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI WA JAMII KATIKA MALEZI NA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO YAONESHA CHANGAMOTO KADHAA BABATI


Na John Walter -Babati
Marafiki wa Elimu wilaya ya Babati wamewasilisha ripoti ya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto.

Ripoti hiyo, iliyowasilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Benjamin Richard, inaonesha changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto katika malezi, usalama, na mazingira ya kujifunzia.

Utafiti huu ulifanyika katika kata nne za Babati ,Bagara, Maisaka na Nangara kwenye shule za Msingi 16, ambapo wadau mbalimbali walihojiwa, wakiwemo watendaji wa kata, wamiliki wa vituo vya kulelea watoto (day care), walimu, wawakilishi wa asasi za kiraia, viongozi wa serikali za mitaa na vijiji, pamoja na wazazi wenye watoto katika shule za awali.
Matokeo Muhimu ya Ripoti

Usalama wa Watoto ShuleniKati ya shule 16 zilizotembelewa, hakuna hata moja yenye uzio, hali inayohatarisha usalama wa watoto.
Shule nyingi zipo karibu na barabara, hivyo kuongeza hatari kwa watoto.

INEC YATOA UFAFANUZI WANAOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA DAR



RAIS DKT. SAMIA ACHANGIA SH. MILIONI 50 KUMUENZI PADRI SHIRIMA


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Seminari Uru, mkoani Kilimanjaro.

Mchango huo umetolewa ili kuweka alama ya kumbukumbu ya kumuenzi marehemu Padri Canute Mkwe Shirima AJ, aliyewahi kuwa Baba Gombera wa shule hiyo, mojawapo ya seminari maarufu nchini.
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alitangaza mchango huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi katika ibada ya mazishi ya Padri Shirima, iliyofanyika Seminari ya Uru, Alhamisi, Machi 20, 2025.

“Haya yote niliyoyasema hapa kumhusu Baba Gombera mstaafu Padri Canute Shirima, alivyokuwa mlezi mzuri akifundisha nidhamu na uwajibikaji, nilimwambia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Thursday, March 20, 2025

RAIS DK.HUSSEIN ALI MWINYI AKABIDHI SADAKA YA IFTAAR KWA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimkabidhi Sadaka ya Iftaar Mwananchi Mkoa wa Kaskazini Pemba. Mukrim Faki Ali, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wete Pemba
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Sadaka ya Iftaar Mwananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Fatma Rashid Said, hafla hiyo ya kukabidhi Iftaar iliyofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wete Pemba.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Sadaka ya Iftaar Mwananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Shuwena Said Ali, hafla hiyo ya kukabidhi Iftaar iliyofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wete Pemba.

WAKOPAJI WAASWA KUTOTUMIA MALI ZA FAMILIA KAMA DHAMANA YA MIKOPO BILA RIDHAA


Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akitoa elimu ya fedha kupitia vipeperushi vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba, uwekezaji, mikopo walizofundishwa wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha kwa baaadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wilayani Butiama, mkoani Mara, yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji Kyankoma, Kata ya Nyamimange, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha yenye mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba na uwekezaji yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC.

TANZANIA NA MISRI KUENDELEZA USHIRIKIANO KWENYE MIRADI YA UMEME -KAPINGA




Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga ( wan ne kushoto) akiwa katika kwenye mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty ( wan ne kulia) tarehe 20 Machi 2025. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, amesema Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme na kudunisha ushirikiano uliowekwa na waasisi wa nchi hizo.
Mhe Kapinga ameyasema hayo leo tarehe 20 Machi,2025, mkoani Pwani wakati alipofanya ziara katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Waziri Badir na ujumbe wake.

‘’Tunamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa msingi imara wa utekelezaji wa miradi huu wa umeme na tumeona matunda halisi ya usimamizi wake.’’ Amsema Mhe.Kapinga

Amesema nchi ya Misri imetekeleza mradi huo wa JNHPP kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya Tanzania ambapo mpaka sasa mashine nane kati ya tisa zimewashwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMEPOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS WA MISRI, IKULU NDOGO YA TUNGUU ZANZIBAR.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Misri Mhe. Badr Abdelatty ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri Waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ( Minister of Foreign Affairs, Emigration and Egyptian Expatriates of the Arab Republic of Egypt ), tarehe 20 Machi, 2025, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Misri Mhe. Badr Abdelatty ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri Waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ( Minister of Foreign Affairs, Emigration and Egyptian Expatriates of the Arab Republic of Egypt ), tarehe 20 Machi, 2025, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalum wa Rais wa Misri Mhe. Badr Abdelatty ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri Waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ( Minister of Foreign Affairs, Emigration and Egyptian Expatriates of the Arab Republic of Egypt ), tarehe 20 Machi, 2025, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

Wednesday, March 19, 2025

TCRA YAKUTANA NA CHAMA CHA BLOGGERS NCHINI (TBN) NA KUAHIDI KUSHIRIKIANA NACHO


MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jumatano tarehe 19.03.2025 imekutana na uongozi wa Tanzania Bloggers Netwark (TBN) katika ofisi za TCRA makao makuu Jijini Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine, TBN imeiomba TCRA kupunguza gharama za usajili wa blogs kama sio kuziondoa kabisa.

Pia TBN imeiomba TCRA iwe inatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa bloggers ili kuwapa ujuzi na uzoefu wa masuala mbalimbali ya kujenga Taifa.
TCRA wamesema kuwa wameyapokea maombi ya TBN na watayafanyia kazi.

"Tunafurahi kukutana nanyi leo, na kujadiliana haya maana Bloggers mna umuhimu mkubwa sana kwenye maudhui ya ndani.

Tuesday, March 18, 2025

TCAA YATAKIWA KUHARAKISHA UJENZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA USAFIRI WA ANGA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Moshi Kakoso akizungumza kuhusu umuhimu wa kukamilisha mradi wa Ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga nchini(CATC) haraka ili kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia, hasa kwa wanafunzi wa kimataifa wakati wa ziara ya Kamati hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza kuhusu namna wizara hiyo ilivyojipanga kusimamia Ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga nchini(CATC) wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipofanya ziara katika ofisi za Mamlaka hiyo Ukonga- Banana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akiwasilisha taarifa ya mradi wa Ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga nchini(CATC) kitakachogharimu takribani bilioni 78 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyofanya ziara katika ofisi za Mamlaka hiyo Ukonga- Banana jijini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI UNGUJA KATIKA IFTAAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi sadaka ya Futari Abdillah Iddi Riziki mkaazi wa Mgeni Haji Wilaya ya Kati Unguja, wakati wa hafla ya Iftaar ya pamoja aliowaandalia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, iliyofanyika katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein SUZA Tunguu jana 17-3-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkaribisha tende Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, kwa ajili ya kufungulia saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakati wa hafla ya Iftaar aliyowaandalia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein SUZA Tunguu Wilaya ya Kati Unguja,iliyofanyika jana 17-3-2025

Monday, March 17, 2025

WAFICHUENI KAUSHA DAMU ILI KUIONDOA JAMII KWENYE MATATIZO


Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Elimu ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akitoa elimu ya fedha kwa wakazi wa Ganyange Wilayani Tarime, Mara, ambapo aliwataka kuwafichua watoa huduma ndogo za fedha wanaofanya kazi kinyume na Sheria, wakati wa zoezi la kutoa elimu hiyo mkoani Mara.
Mchumi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Glory Uiso, akitoa ufafanuzi wa taarifa zilizo kwenye kipeperushi kuhusu elimu ya fedha Wilayani Tarime, wakati wa zoezi la kutoa elimu kwa wananchi wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKAMU MWENYEKITI WA BENKI YA DUNIA BI. VICTORIA KWAKWA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, tarehe 17 Machi 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

WADAU AFRIKA WAKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI NAMNA YA KUUNGANISHA MIFUMO YA USAFIRI WA ANGA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizungumza
na wadau mbalimbali wa sekta ya anga kutoka zaidi ya nchi 13 za Afrika wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mfumo wa Uboreshaji wa Usafiri wa Anga (ASBU) 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Huduma za Urambazaji wa Anga (ANS) katika Shirika la Usimamizi wa Usalama wa Anga la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-CASSOA) Sylvestre Sinarinzi akitoa shukrani kwa Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa warsha hiyo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika maendeleo ya sekta ya anga wakati wa ufunguzi wa Mfumo wa Uboreshaji wa Usafiri wa Anga (ASBU) 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam.

DIWANI WA KATA YA MSHANGANO AJIUZULU


Diwani wa Kata ya Mshangano ,Samuel Mbano akionesha barua ya kujiuzulu
Diwani wa Kata ya Mshangano ,Samuel Mbano aliyejiuzulu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Ruvuma.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya James Danny Mgego akithibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa diwani wa Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma

Na Regina Ndumbaro Ruvuma.
Diwani wa Kata ya Mshangano katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, Samuel Mbano, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya udiwani.

SERIKALI: TUMIENI MIKOPO KUWEKEZA KWENYE BIASHAR ZINAZOZALISHA


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji cha Suguti wakifuatilia elimu iliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Suguti, Musoma, mkoani Mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Bw. Msongela Palela, akizungumza na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha iliyofika mkoani Mara kwa lengo la kutoa elimu ya fedha katika maeneo mbalimbali mkoani humo. Kushoto ni Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mzava na kulia ni Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizaya ya Fedha Bw. Santley Kibakaya na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Bi. Angela Mollel.