ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 15, 2010


Aiba mtoto kwa style na kusingizia kujifungua
Mwanadada mmoja aliyetambulika kwa jina la Agnes John,mkazi wa Olmatejoo,Arusha..anashikiliwa na watoto wa afande mwema (Polisi) akidaiwa kuiba mtoto wa miezi 4.

Story yenye iko hivi...Agnes alifika kwa mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Zainabu Ramadhani, ambaye ni muuza mahindi mahindi ya kuchoma na kununua mahindi huku akitoa noti ya msimbazi 'elfu kumi'.

Kutokana na Zainabu kutokuwa na chenji ndipo alipomkabidhi mtoto wake wa miezi minne Ramla Mohamed kwa Agnes ili amlindie wakati anaenda kusaka chenji kitaa cha karibu.

Aliporejea baada ya dakika tano, mama huyo hakuwepo na mtoto huyo na ndipo alipokwenda Kituo Kikuu cha Polisi na kutoa taarifa za kupotea kwa mtoto huyo.

Baada ya kuiba mtoto huyo, mama huyo alikwenda katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na kujifanya anaumwa kutokana na uzazi na kupiga simu kwa rafiki yake wa kiume, Hamisi Ramadhani na kumwambia amejifungua mtoto wa kike.

Wifi zake walipofika katika hospitali hiyo walimkuta akiwa na mtoto huyo ambaye alikuwa na miezi minne na kuanza kuhoji iweje ajifungue mtoto mkubwa kiasi hicho.

Ilielezwa kuwa baada ya kutokea mtafaruku mkubwa hospitalini hapo, mawifi hao walitoa taarifa polisi na mwanamke huyo kubainika kuiba mtoto huyo ambaye amerejeshwa kwa mzazi wake na uchunguzi zaidi ukiendelea.

No comments: