ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 15, 2010

David Beckham
Matumaini ya kiungo wa kati wa AC Milan David Beckham kuchezea Uingereza katika kombe la dunia kwa mara ya nne, sasa yameanza kufifia.
Beckham anauguza jeraha la kisigino, alilopata wakati wa mechi kati ya AC Milan na Chievo. Nyota huyo wa soka alikuwa akijaribu kuugonga mpira wakati alipoumia.
Beckham anatumaini kuwa ataweza kuwa mchezaji wa kwanza wa timu ya Uingereza kucheza katika mechi za kombe la dunia mara nne mfululizo.
Lakini tayari ameelezea wasiwasi wake kuwa huenda akakosa nafasi ya kuchezea nchi yake . Amekiri kwamba itambidi kutia bidii zaidi kujishindia nafasi katika timu itakayosafiri kuenda Afrika kusini, mwezi wa sita.

No comments: