Bil. 90/- zatumika kuwalipa walinzi wa Kiwira
na Moses Ng?wat, Mbeya [Photo] WAFANYAKAZI wa kampuni ya ulinzi ya New Imara Security wanaolinda mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira wanalipwa malimbikizo ya mishahara ya miezi 19.Malipo yamefanywa na serikali kwa kile kinachodaiwa kuwa ni shinikizo la walinzi hao waliotishia kugoma kuendelea na kazi hadi hapo watakapolipwa mishahara ya miezi 19 ambayo walikuwa wakimdai mwajiri wao.
Mkurugenzi wa New Imara Securty, Essau Kamwela, alisema walichowalipa walinzi hao ni sehemu ndogo ya malimbikizo ya wafanyakazi hao kwa sababu serikali imeshindwa kulipa kiasi kilichotakiwa.
Wakizungumza na gazeti hili mgodini hapo wafanyakazi hao walisema wameamua kupokea kiasi hicho kidogo kwa kuwa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Walisema hata hivyo malipo ya mishahara yao inakinzana na waraka wa serikali juu ya ajira wa kutaka wafanyakazi wa migodini walipwe shilingi 450,000 ambapo wamekuwa wakilipwa chini ya hapo.
“Mgodi huu ambao ni kati ya rasilimali za taifa, wafanyakazi wa sekta hii ya ulinzi wasipolipwa vizuri hali inaweza ikawa mbaya zaidi mgodini hapa, kwa kutambua umuhimu wa watumishi hawa,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Hii ni mara ya pili kwa serikali kuwalipa wafanyakazi wa mgodi huo ambapo mwaka jana iliwalipa zaidi ya wafanyakazi 500 waliokuwa wakiudai uongozi wa mgodi huo
No comments:
Post a Comment