ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 27, 2010

Rais Mubarak arejea nyumbani

Rais Mubarak amereja nyumbani baada ya matibabu
Rais Hosni Mubarak wa Misri amerejea nyumbani kutoka Ujerumani, ambako alifanyiwa upasuaji kuondoa kibofu nyongo na uvimbe katika utumbo mdogo.
Televisheni ya taifa ya Misri ilionyesha moja kwa moja kuwasili kwa Rais Mubarak katika mji wa Sharm el-Sheikh ambako maafisa wa serikali na viongozi wa kijeshi walikuwa wanasubiri kumpokea.
Bw. Mubarak mwenye umri wa miaka 81 alikuwa anapumzika nchini Ujerumani ili kupata nafuu kufuatia upasuaji huo katika hospitali ya chuo kikuu cha Heidelberg.
Daktari wake Markus Buechler amesema Rais huyo sasa amepona kabisa.
Hata hivyo daktari huyo amesema kwenye taarifa yake kwamba amependekeza Rais Mubarak aendelee kupumzika nyumbani ili kupata nafuu zaidi katika kipindi cha majuma mawili yajayo, kabla ya kuanza kurejea kwa utaratibu kwenye shughuli zake za kila siku.

No comments: