Bunge la Uingereza linatarajiwa kufanya kikao cha dharura baadaye leo kujadili juu ya ghasia ambazo zimekumba miji kadhaa nchini humo.
Waziri Mkuu David Cameron atawasilisha taarifa ya serikali pamoja na harakati za polisi katika kuthibiti ghasia na uporaji.
Hii ni mara ya tano wabunge Uingereza wamelazimika kukatiza likizo zao katika miongo mitano.
Waziri Mkuu David Cameron imekuwa mara yake ya pili kuitisha kikao cha dharura aliwa madarakani, awali ikiwa kujadili sakata ya udukuzi wa simu.
Tukio la sasa linaonekana kuwa na uzito mkubwa.Kila serikali ina wajibu mkubwa kuhakikishia wananchi wake usalama pamoja na utekelezwaji wa sheria.
Changamoto kubwa inayomkabili David Cameron ni kuishawishi bunge kwamba serikali yake imeweza kuthibiti hali kwa sasa.
Cameron ametaja machafuko ya sasa kama vitendo vya jinai na kutowajibika wala siyo kero za tofauti za kijamii na gharama za maisha.
Msimamo huu unaonekana samba mba na maoani ya raia wengi, japo wamelaumu serikali hususan idara ya polisi kwa kutochukua hatua madhubuti kukabiliana na
makundi yaliyozua rabsha na kupora mali.
Polisi wamekuwa wakishika doria katika miji ya Uingereza kuzuia tukio jingine.Kwa sasa hali ya utulizu umerejea kutokana na idadi ya polisi wanaoshika doria
pamoja na mvua kubwa ambayo imenyesha maeneo yaliyoathirika.
Tayari Waziri Mkuu amesema njiya mbadala za kuzima ghasia zitatumiwa ikiwemo maji ya kuwasha.
Bw. Cameron amezuru mji wa Birmingham kufariji familia za watu watatu waliogongwa na gari wakati wakijaribu kulinda mali zao.
No comments:
Post a Comment