ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 12, 2011

Harambee UK ya kusaidia wahangwa wa Mv spice Islander




Jumuiaya ya Watanzania nchini Uingereza TANZ-UK  ikishirikiana na TANZ-UK Jumuiya ya Wanzanzibar waishio Uingereza (ZAWA) Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa fundrising maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.

Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi  na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba  mwenye  fedha au chochote kile  cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na  kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana  itakuwa sehemu ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.
 anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni saa nane mchana (2pm sharp).
Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na ............... Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565, ZAWA 07538063536,TA London 07404332910 
 UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA, 
Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki Watanzania wote popote pale walipo duniani.

ASANTENI
 MWENYEKITI, 
TANZ-UK

No comments: