ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 4, 2013

WAKATI WA UKWELI UMEWADIA KATI YA WAGHANA RICHARD COMMEY NA BILAL MOHAMMED

For Immediate Release                                      Media Contact: Onesmo Ngowi

IBF/Africa Notes 17                                             Tel:(+255) 754- 360828


International BoxingFederation Africa
IBF/AFRICA
FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 1st, 2013 -Dar-Es-Salaam, TANZANIA-Ule wakati wa ukweli uliokuwa unangojewa kati ya ni nani haswa atayekuwa ubingwa wa uzito mwepesi (lightweight) katika bara la Afrika kati ya Richard Commey na Bilal Mohammed wote mabondia kutoka Ghana umewadia na sasa zimebaki siku tatu (3) tu. Mabondia hao ambao wamekuwa wanajifua kweli kweli kwenye fukwe mbalimbali za jiji la Accra, watapanda ulingoni siku ya Jumamosi tarehe 8 Machi katika mpambano ambao unategemewa kuwa waburudani tosha kutokana na ujuzi wa wote wawili.

Richard Commey (kushoto) akimshindilia konde zito mpinzani wake nchini Uingereza

Promota wa Richard Commey bwana Michael Amoo-Bediako ambaye anaishi nchini Uingereza na anayemiliki klabu nyingi za afya (Health Clinics) pamoja na kumbi za kufanyia mazoezi (Gymnasiums) katika nchi mbalimbali za Ulaya ana matumaini makubwa sana ya kuinua viwango vya mabondia wa Afrika akitumia mabondia wa Ghana.

Bediako amekuwa anamfanyia mazoezi makali sana Richard katika jiji la London nchini Uingereza ili kuinua kiwango chake cha ngumi na akiwa huko ameweza kuwasambaratisha mabondia wengi wa Ulaya na Asia.

Bwana Bediako ametumia pesa nyingi sana kuhakikisha kuwa Afrika inaonyesha kiwango kikubwa katika ngumi na amedhamiria kuamdaa mapambano kila mwezi.

Suali kubwa ambalo limo katika vichwa vya wadau wengi wa ngumi katika nchi ya Ghana na nchi zote za Afrika ya Magharibi ni Je? Nani kati ya wawili hawa ataibuka kuwa Mfalme wa uzito mwepesi barani Afrika?
Suali hili lenye thamani ya dola bilioni moja halitangoja kupata jibu muda mrefu kwani ni siku tatu tu kuanzia sasa litajibiwa nayo tarehe 8 Machi, 2013.

Imetolewa na:


ISSUED BY:


INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)

DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

No comments: