Nembo ya Asasi isiyo ya kiserikali ya CITYarts inayojishughulisha na kueneza amani kupitia sanaa ya uchoraji unaofanywa na watoto kutoka mataifa mbalimbali duniani
Na Mwandishi Maalum
Imeelezwa kwamba ujumbe wa amani unaweza kuenezwa kwa njia
nyepesi na rahisi kama ile ya kuwatumia
vijana na watoto kutumia vipaji vyao kuchora michoro inayobeba ujumbe unaosisitiza umuhimu wa
amani duniani.
Hayo yameelezwa na Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya miaka mitano ya “Jioni ya
Amani”, ambapo Asasi isiyo ya
kiserikali ijulikanayo kama CITYarts
Pieces for Peace ilionesha kwa wageni
waalikwa michoro mbalimbali iliyochorwa na watoto kutoka nchi 62 zikiwamo za
Afrika.
Madhumuhi ya hafla hiyo ambayo Ubalozi ulikuwa mwenyeji yalilenga katika
kuonesha ni kwa namna gani watoto wanavyoweza kuhuburi na kuienzi amani kupitia sanaa ya uchoraji na kwa njia hiyo pia kukuza vipaji vyao.
Kwa maelezo na picha zaidi bofya read more
CITYarts Pieces for
Peace ambayo makao yake yako New York,
imekuwa ikitembelea nchi mbalimbali, na kuwahamasisha watoto na vijana kuchora
iwe kwenye makaratasi, mabango au hata kuta kwa lengo moja tu la kueneza ujumbe wa amani.
Balozi Manongi amewashukuru waandaaji wa hafla hiyo
kwa kubuni wazo hilo jema la
kuwahamasisha watoto kutumia vipaji vyao vya uchoraji kuhubiri
amani hasa kwa kuzingatia kwamba mara nyingi mawazo wanayotoa watoto yanakuwa
hayajachakachuliwa.
Naye Mkurugenzi wa CITYartsPieces for Peace, Bi
Tsip Ben-Haim pamoja na kuushukuru
Ubalozi wa Tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa hafla hiyo,
amesisitiza haja na umuhimu kwa jumuia
ya kimataifa kuienzi amani kwa hali na
mali.
Akasema kwamba uamuzi
wa Asasi yake wa kuanzisha program hiyo ya kuwashirikisha watoto kupitia sanaa
kueneza ujumbe wa amani, imekuwa na mafanikio sana na kwamba program hiyo imesambaa katika nchi nyingi.
Michoro wanayochora
watoto na vijana hukusanywa na kuwekwa katika mabango ambayo waandaaji wa
michoro hiyo husafiri nayo kila nchi
wanayokwenda na kuionesha kwa watu
wengine na kwa namna hiyo kueneza ujumbe wa amani kutoka taifa moja hadi taifa jingine.
Baadhi ya Michoro hiyo ambayo watoto kutoka nchi mbalimbali wamechora kama mchango wao katika kueneza ujumbe wa amani
Ujumbe wa amani katika michoro
wageni waalikwa wakisoma ujumbe wa amani
watoto hawa Linda, Maria, Stephen na Alex nao walipata fursa ya kutoa ujumbe wao wa amani kwa njia ya michoro, michoro hapa wapo bize kila mmoja akichora ujumbe wake alioubuni mwenyewe.
Stephen, Maria na Linda wakiwaonyesha wageni waalikwa ujumbe ambao kila mmoja ameuchora, michoro yao hiyo baadaye itaunganishwa na ya watoto wengine.
Na utamduni wetu ulikuwapo, watanzania hawa, Eri Fungo na Amiri Koba hawakuwa nyuma kurindimisha midundo iliyosherehekesha hafala hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa CITYart akielezea madhumuni ya hafla hiyo na kubwa zaidi ushirikishwaji wa watoto katika kueneza ujumbe wa amani
wageni waalikwa wakipata kitu kidogo walichangamkia sana Maandazi
Balozi Tuvako Manongi akiwashukuru waandaji wa hafla hiyo pamoja na wageni waliofika, katika mazungumzo yake mafupi, Balozi alisititiza kwamba watoto na ambao mawazo yao hayajachakachuliwa.
Sehemu ya wageni waalikwa
No comments:
Post a Comment