Mkuu wa Kitengo Cha Ukaguzi wa Mikataba katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.
Steven H. Issack alipotembelea banda la wizara ya fedha kutaka kupata ufafanuzi
juu ya uanzishwaji wa mikopo kwa watumishi wa umma kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa
Serikali, kutoka kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Mikopo Bi. Christine Ngonyani na kulia ni Bi. Miriam Mnzava Nchini
Ghana.
Mkuu wa Kitengo cha
Mikopo wa Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine
akiwaeleza wananchi wa Ghana jinsi idara ya
Mhasibu Mkuu wa Serikali inavyosaidia Watumishi wa Umma katika kupata
Mikopo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina
O. Kombani alipotembelea Banda la Wizara ya fedha katika Maonesho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma.
Washiriki kutoka Nchi mbalimbali walipotembelea katika makumbusho ya
taifa ya Ghana.
Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Utumishiwa Umma kutoka Tanzania na nchi
nyingine wakifurahia ushiriki katika maonesho hayo Nchini Ghana.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha chini ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi.
Miriam Mnzava alipotembelea banda la Zimbabwe wakati wa maonesho hayo.
Msemaji wa Wizara ya
Fedha akiwa ameambatana na washiriki wengine kutoka wizara ya fedha wakiwa
kwenye banda la Zimbambwe wakibadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi katika
nyanja mbalimbali walipokuwa Nchini Ghana.
Afisa Tawala
Mwandamizi Bw. E. Ndofi kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha,
akitoa ufafanuzi kuhusu watumishi wa Idara na Vitengo vilivyopo kwa Mhasibu
Mkuu wa Serikali wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana
Picha zote na Scola Malinga-Wizara ya fedha, Tanzania
No comments:
Post a Comment