ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 28, 2014

MTOTO WA MIAKA MINNE APOTEZA MAISHA BAADA YA KUDUMBUKIA CHOONI


Mwili wa mtoto John Mwapwani aliyefariki majira ya  asubuhi baada ya kudumbukia kwenye tundu la choo nyumbani kwao kata ya Chemchem eneo la Aly Hassan Mwinyi mtaa wa Sikanda Manispaa ya Tabora.Maelezo ya awali,mtoto huyo mara baada ya kuamka asubuhi baba yake mzazi alimwambia aende chooni kujisaidia kama ilivyo ada kwa wazazi wafanyavyo kwa watoto wao,Mtoto John(4)alikwenda chooni na kimya cha muda mrefu baadaye baba yake alimfuata na kukuta mwili wake ukielea kwenye maji machafu akiwa tayari amepoteza maisha.

1 comment:

Anonymous said...

jamani inasikitiha sana...na ilo shimo walitengeneza pana vip kwani naona wengine kule vijijini wanafanya lembamba hata mtt kudumbukia si rahisi,poleni sana.