ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 3, 2014

ALICHOANDIKA ZITTO KABWE BAADA YA KUMZIKA MAMA YAKE MZAZI JANA.




Tumempumzisha mama kwenye nyumba yake ya milele,jirani na alipopumzishwa baba yake mzazi. Nawashukuru sana nyote kwa salam zenu za pole.

Nawashukuru nyote mlioweza kufika kigoma kumsitiri mama. Sina cha
kuwalipa, mola atawalipa.Nawashukuru sana wakazi wa Manispaa ya Kigoma, jimbo la Kigoma Kaskazini na wana Kigoma wote.Nawashukuru watanzania. Madaktari wote waliomhudumia mama, wahudumu wa hospitali, maafisa wa Bunge na wabunge wenzangu. Mola awazidishie katika shughuli zenu.

Mama yangu alikuwa nguzo kubwa kwangu na familia yetu. Mti mkubwa umeanguka. Mola amempenda zaidi mama. Pumzika kwa Amani.

1 comment:

Anonymous said...

pole sana zitto kwabwe Allah akupe moyo wakustahamili na family yako yote kazi ya Allah haina makosa stahamili baba upate kubarikiwa.

Allah Amghufiriyee yeye pamoja na wazee wetu wote na ndungu na jamaa walipo mbele ya haki. Amin