Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando wakati akiwasili ofisi ya mkoa huo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa serikali mkoani hapo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando (kushoto), akitoa taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Paul Chagonja akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo yenye lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo kwa lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu
kulia),akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando,(wapili kulia). Naibu Waziri
alifika mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za
masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi. Wengine ni viongozi wa
mkoa huo kutoka kada mbalimbali.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment