Advertisements

Wednesday, February 22, 2017

Majambazi yaua OCCID wa polisi Kibiti

By Azory Gwanda, Mwananchi

Kibiti. Watu watatu akiwamo OCCID wa Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na watu wadhaniwa kuwa ni majambazi katika Kijiji cha Jaribu wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gullamuhusein Kifu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto walikivamia kituo cha Wiley's cha kukusanyia ushuru kilichopo kijijini hapo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatano ambapo watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki walivamia kuzuizi cha maliasili kilichopo kijijini hapo na kukichoma moto kabla ya majibizano ya risasi na polisi waliokuwa doria kwenye eneo hilo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mchukwi, Zakaria Lukeba amethibisha kufikishwa kwa mwili wa Kubezya ukiwa na jeraha la risasi tumboni pamoja na maiti mbili ambazo hazijajulikana majina.

No comments: