Advertisements

Monday, September 24, 2018

RAIS DKT MAAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA STIEGLER"S GORGE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge wakisimama kwa dakika kadhaa kuwakumbuka marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza Septemba 20, 2018. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kwa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge pamoja na wataalamu wakati wa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.

No comments: