Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akikagua gwaride la
heshma alilioandaliwa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi wa NCAA
alipowasili uwanja wa ndege wa Ngorongoro kwa ziara ya kikazi katika
eneo hilo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (wa tatu kutoka
kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Kamishna wa NCAA Dkt.
Christopher Timbuka (wa pili kutoka kulia) kuhusu ukarabati wa Barabara
ya kutoka eneo la Seneto hadi Golini yenye urefu wa Km 88, wengine ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela (wa pili kulia) Mkurugenzi wa
Idara ya Wantamapori Dkt. Mauruce Msuha (kulia) na Naibu Kamshna wa NCAA
Huduma za Shirika Bw. Needpeace Wambuya (Kushoto)
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (kulia)
akimsikiliza Naibu Kamishna wa NCAA Dkt. Christopher Timbuka kuhusu
juhudi za NCAA katika kuhifadhi, kulinda na kuendeleza shughuli za
Utalii zinazofanyika katika Hifadhi ya Ngorongoro
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Wanne kutoka kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela (wa nne kutoka kulia), Viongozi wa NCAA na Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika geti la kuingia eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wakati wa ziara ya Mhe. Waziri
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akielezea kufurahishwa na juhudi za Uhifadhi, utalii na ukarabati wa Miundombinu ya barabara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro
Na Mwandishi wetu, NCAA.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana tarehe 6 aprili,
2022 amefanya ziara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na Loliondo
Mkoani Arusha kwa lengo la kukagua shughuli za Uhifadhi, Utalii na
miradi mbalimbali ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Katika
ziara hiyo Mhe. Chana ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA) kwa juhudi za uhifadhi wa mazingira, ulinzi wa wanyamapori,
ujenzi wa miundombinu na kuimarisha huduma za utalii kwa wageni
wanaotembelea eneo hilo.
“Nimetembelea eneo la Hifadhi ya
Ngorogoro na Loliondo ili kujionea kazi kubwa inayofanywa ya kuhifadhi,
kulinda Wanyamapori, kuendeleza shughuli za utalii na ukarabati wa
miundombinu ambayo serikali imekuwa ikitoa fedha, nashukuru uongozi wa
NCAA unasimamia vizuri na nimeona kazi kubwa inaendelea kufanyika”
alifafanua Dkt. Chana.
Mhe. Waziri ameongeza kuwa Serikali
itaendelea kuhakikisha Hifadhi ya Ngorongoro inalindwa kwa njia zote
kama moja ya maeneo muhimu ya urithi wa dunia na chanzo cha mapato ya
Serikali yatokanayo na shughuli za Utalii hivyo ni muhimu kulindwa na
kuhifadhiwa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha,
Dkt. Chana ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa za kutangaza vivutio
vya Utalii kupitia filamu ya The Royal tour inayotarajiwa kuzinduliwa
hivi karubuni.
Ametoa wito kwa watanzania kuunga mkono juhudi za
kutangaza vivutio kwa wadau mbalimbali na kutenga muda kutembelea
vivutio hivyo ili kuongeza hamasa ya utalii.
Vilevile Mhe. Waziri
ametembelea bonde la Kreta ya Ngorongoro na kufurahishwa na shughuli za
uhifadhi zilizochangia ongezeko la Wanyama. “Katika eneo la kreta
nimeona Faru zaidi ya 8, Tembo, Nyati, Simba na wanyama aina mbalimbali,
naomba tuendelee kutunza, kuhifadhi, kulinda na kudhibiti shughuli
ambazo zinaweza kuharibu mazingira na ikolojia katika eneo hili”
ameongeza Mhe. Pindi Chana.
Katika hatua nyingine Mhe. Waziri
ametembelea sehemu ya barabara ya kutoka Hifadhi ya Ngorongoro hadi
Golini ambapo ni mpaka wa Hifadhi ya Serengeti kwa lengo la kukagua
ukarabati wa Miundombinu ya barabara utokanao na fedha za maendeleo kwa
ustawi wa Taifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 zilizotolewa na Serikali.
Kupitia
mpango huo NCAA ilipokea jumla ya shilingi Bilioni 6.2 kwa ajili ya
ukarabati wa barabara na ununuzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ambapo
ukarabati huo utawezesha barabara kupitika msimu wote wa mwaka na
kuongeza tija kwenye shughuli za utalii ndani ya Hifadhi.
Katika
ziara hiyo Mhe. Waziri ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John
Mongela, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha, pamoja na
Viongozi wa NCAA.



No comments:
Post a Comment