Friday, January 2, 2015

YANGA VETERANI YATWAA KOMBE LA PSPF BAADA YA KUINYUKA SIMBA VETERANI

Nahodha wa timu ya maveterani wa Yanga, Salvatory Edward, akipokea kombe kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, baada ya kuinyuka Simba Veterani kwa penati 5-4 kufuatia sare ya mabao 1-1 katika pambano la bonanza lililodhaminiwa na mfuko huo na kupigwa kwenye uwanja wa Bandari Tandika, wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam jioni Alhamisi Januari 1, 2015. Kufuatia ushindi huo Yanga veterani pia walijinyakulia kitita cha shilingi milioni 1, wakati watani wao wa jadi Simba, shilingi laki 5
Kipa wa Yanga, Peter Manyika akichupa kuunyaka mpira uliopigwa kwa shuti kali na mshambuliaji wa Simba
Dua Saidi wa Simba, (Kushoto), akiondosha mpira kwenye hatari
Kocha wa Simba veterani George Lucas "Gaza" akiwahimiza wachezaji wake
Bakari Malima "Jembe ulaya", (Kushoto), wa Yanga, akikokota mpira huku aiwindwa na mchezaji wa Simba
Kocha wa Yanga veterani, Peter Tino, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Madaraka Selemani mzee wa Kiminyio, akikokota ngoma
Makumbi Juma, homa ya jiji, akiwa kwenye benchi la ufundi la Yanga, akionekana kutoa maelekezo
Peter Tino
Salvatory Edward

4 comments:

Anonymous said...

doo nimeipenda sana hii

Anonymous said...

duuu unakumbusha mbali sana

NYE said...

Hizi ndiyo zilikuwa Yanga na Simba za ukweli.....licha ya kucheza kwa mapenzi wamebakia kuwa masikini.

Anonymous said...

Dah enzi zetu hizo