Friday, January 8, 2016

WAZAZI/WALEZI WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari Katika ukumbi wa Maendeleo ya Jamii, Jisia, wazee na watoto jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuhamasisha wazazi au walezi kuwahamasisha waoto kujiunga na shule za Msingi na Sekondari kwa 2016.
kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SERIKALI itawafungilia mashtaka na kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi wote watakashindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto shule ili kupata Elimu ya Msingi na Sekondari.
Pia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ikishirikiana na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi, Technologia, na Ufundi inawahamasisha wazazi au walezi kutimiza wajibu wao kuhakikisha kuwa watoto wenye umri wa kuanza shule za msingi na Sekondari kuanza kwa wakati.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pia viongozi na watendaji wa mikoa na halmashauri,  maafisa Maendeleo ya jamii na watendaji wa kata wameaswa kusimamia na kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha wanahamasisha jamii ipasavyo juu ya watoto kujiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka huu.
Ummy amesema kuwa maafisa wa maendeleo ya jamii za mikoa, Halmashauri na kata  zote hapa nchini watoe taarifa za utekelezaji wa jambo la watoto kwenda shule mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Aidha  Serikali inatoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wote wanaendelea na masomo ya shule ya Msingi na Sekondari vizuri na wahudhurie masomo yao kwa ufanisi, pia serikali haitegemei kuona utoro wa watoto mashuleni kutokana na sababu zinazoweza kuepukika.


No comments: